GET /api/v0.1/hansard/entries/1119542/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119542,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119542/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda. Ndiyo maana nilikuwa ninataka kumwarifu Seneta wa Mombasa. Tulikutana na hao mawakala ambao wako katika vikundi viwili, ambapo wamejisajili pamoja, kama association . Tuliwasikiliza na pia wale wafanyikazi ambao wako kule. Ndiyo maana tumependekeza katika ripoti hii ya kwamba hao mawakala wote wapigwe msasa, ili kudhibitisha ya kwamba wanafanya kazi yao kupitia sheria iliyopo, katika NationalEmployment Authority Act na huo msasa ukipigwa, waweze kusajiliwa upya na serikali. Kuna wengi kama yule ambaye amemtaja, ambao kukitokea shida anarusha mikono juu. Hataki kuwajibika wala kumsaidia yule msichana. Hayo ni licha ya kuwa wamepewa pesa, hata zile za kuweka bima na kuhakikisha kwamba yule msichana ambaye ameenda kufanya kazi kule nje ako na tiketi au nauli ya kurudi akipata shida kule Uarabuni."
}