GET /api/v0.1/hansard/entries/1119863/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1119863,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1119863/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Taarifa iliyoletwa siku ya leo na Sen. Cherargei ni nzuri. Mambo ya mbolea yamekuwa kizungumkuti katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu ukiangalia bei yake imeongezeka maradufu ilhali ukiangalia wakati huu ugonjwa wa Korona umewaadhiri watu wengi kwa njia nyingi sana. Kwa hivyo, hawawezi kujimudu hata kununua ile mbolea. Mbolea inahitajika kwa kupanda chochote ambacho unataka kupanda ili uweze kupata mavuno bora. Kamati ambayo itaangalia haya mambo iangazie kwa kindani ili tuweze angalau kuwapa wakulima wetu afueni. Ukienda Kaunti ya Laikipia, utaona watu wanapanda mahindi, ngano na nyanya wanategemea mbolea. Hata ingawa bei ya mbolea imeongezeka maradufu, bei ya mavuno haiongezeki. Kwa hiyo, wakulima wetu wanaendelea kusoneneka na kuwa na shida nyingi. Kwa hivyo, tunaomba ya kwamba kamati iangalie haya mambo kwa kindani na iweze kuwapatia angalau afueni wakulima wetu kwa sababu ukulima ndio uti wa mgongo wa maendeleo nchini ya Kenya. Nchi yetu inajulikana kwa sababu inategemea ukulima. Ikiwa kamati yetu haitafanya hivyo, tutaonekana kama tumelemewa na kazi ambayo tunapaswa kufanya. Tuwasaidie wakulima ili tukuze uchumi. Asante sana, Bi Naibu Spika."
}