GET /api/v0.1/hansard/entries/1120158/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120158,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120158/?format=api",
"text_counter": 426,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia ripoti ya Kamati ya Ajira na Huduma za Jamii ya Bunge la Seneti kuhusiana na wafanyikazi wanaofanya kazi ughaibuni hususan Mashariki ya Kati. Hiyo ni katika nchi za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar na nyingine ambazo ziko eneo hilo kama Kuwait na kwingineko. Kwanza, ningependa kuipa kongole kamati hii kwa kuweza kulizamia jambo hili na kuja na ripoti ambayo inaridhisha kabisa. Nimeweza kuisoma kwa mtazamo fagia ripoti hii. Japo kuwa nimesikia Maseneta kadhaa wakisema kwamba kuna pendekezo la kusimamisha uajiri huu kwa muda wa miezi sita, nimeangalia ukurasa wa nane wa ripoti hii ambayo inazungumzia mapendekezo. Sikuweza kuliona pendekezo hilo. Bw. Spika wa Muda, pendekezo kama hilo litaletea athari mbaya nchi yetu kwa sababu kazi hizi sio kwamba zinakuja Kenya pekee yake. Kazi hizi nizakwenda kila sehemu ulimwenguni. Wengi wa wale watoto wetu na ndugu zetu ambao wanapata ajira kama hizi wataweza kuzikosa kwa huo muda wa miezi sita ambao umeweza kupendekezwa ili mambo yaweze kurekebishwa."
}