GET /api/v0.1/hansard/entries/1120165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120165,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120165/?format=api",
"text_counter": 433,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, na Sen. Sakaja. Ajira ughaibuni imekuwa ni sehemu kubwa ya mapato ya nchi yetu na pia kwa familia za wahusika ambao wanafanya kazi hizi. Kazi hizi zimekuwa siku nyingi sana. Kutoka jadi, Mombasa imekuwa na watu wanafanya kazi ughaibuni; Uarabuni na kwingineko kwa muda mrefu. Hizi kesi ambazo zinakuja sasa za watu kudhulumiwa haki zao na vile vile kuteswa na kuwekwa katika hali ya utumwa zimeongezeka kwa siku za karibuni. Baadhi ya sababu ya kuongezeka kwa kesi hizi ni kuwa wanaokwenda kufanya kazi hizi wameongezeka kwa kirefu kiasi ambacho ni watu wengi wanaweza kuenda sasa kufanya kazi hizi kuliko ilipokuwa pale awali. Bw. Spika wa Muda, jambo la pili pia ni kwamba watu wengi sasa wame elimika kidogo kuhusiana na haki zao za kikatiba na kikazi. Utapata watu wengi wanaweza kuja na kulalamika kuhusiana na mambo haya. Jambo la tatu ni kwamba kuna tofauti ya mila na tamaduni za wale watu ambao wanatoka Kenya kuenda kufanya kazi hizi na wenyeji wao kule sehemu wanakofanya kazi. Wengi wa kule wanazungumza lugha ya Kiarabu. Ni wachache wanaweza kuzungumza Kiarabu na Kiingereza. Unapata kwamba watu wetu wa Kenya wanazungumza Kiswahili na Kiingereza. Kwa hivyo, wanapofika kazini kule wanapata shida ya kuwasiliana na waajiri wao kwa sababu ya ukosefu wa lugha ya Kiarabu. Bw. Spika wa Muda, pia wengi wanaochukuliwa wakishalipa zile pesa zinazo takikana ya dalali ama walaka wanapandishwa ndege kuenda kule kufanya kazi bila ya kufanyia mafunzo yeyote ya vitu watakwenda kufanya kule kazini. Hii ni ile atakapokwenda kule ajue matarajio yake ni nini na matarajio ya mwajiri wake ni nini."
}