GET /api/v0.1/hansard/entries/1120296/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120296,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120296/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Taarifa iliyoletwa katika Seneti na Sen. Mwaruma na maombi ya Taarifa iliyoletwa katika Seneti na Sen. (Dr.) Langat. Kazi ya walimu ni muhimu sana katika nchi yetu kwa sababu wanajenga msingi wa wanafunzi wetu kutoka mwanzo wa masomo yao mpaka watakapomaliza katika chuo kikuu au kwingineko. Taaluma ya ualimu ni lazima itiliwe maanani sana na Serikali. Tumeona hivi majuzi walimu wamenyimwa nyongeza ya mshahara kwa karibu miaka mitatu inayokuja, kwa sababu inasemekana uchumi umezorota. Papo hapo, tunaona kwamba wako tayari kuwabandikia mzigo wa kujisomesha kwa gharama kubwa ya Kshs150,000 ambayo ni gharama tu ya kulipia kozi bila ya labda chakula na malazi. Kwanza, Wizara ya Elimu kabla ya kuleta huu mtaala mpya, lazima walikuwa wamefanya utafiti na kujua kwamba walimu watahitaji ujuzi upi mpya kuwawezesha kusomesha mtaala huo. Je, huu mtaala ambao wameuleta ulipitia ushirikishwaji wa uma ili yale ambayo yatakubalika yawe ni rahisi kutekelezwa katika siku za usoni? Hivi sasa, karibu kila kaunti ina chuo kikuu. Hatuoni sababu ya mtaala huu kufundishwa na vyuo vinne pekee. Hili si jambo tunaloweza kusema lina utaalamu maalum ambao unaweza kupatikana katika chuo kimoja pekee. Ni mtaala unaoweza kufundishwa katika chuo kikuu chochote katika nchi ya Kenya, kwa sababu ni walimu kupewa mafunzo mapya kuhusu watakavyotekeleza huo mtaala mpya. Mwisho, walimu kote nchini tayari wanafundisha. Je, kwa wale ambao hawatakuwa tayari, kwa mfano, hawana pesa za kusoma huu mtaala mpya, je, watafutwa kazi ama watafanywa nini? Ni wazi kwamba wengine hawatakuwa na uwezo wa kifedha wa kwenda kufanya mtaala huu mpya."
}