GET /api/v0.1/hansard/entries/1120833/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120833,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120833/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Wengi waliotangulia wamejaribu kulaumu mapatano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Mhe. Raila Odinga. Lakini Hoja kama hii hausiani na majukumu ya waliowengi na waliowachahe katika Bunge hili. Mbunge ama Seneta yeyote alikuwa na uwezo na fursa ya kuleta Hoja hii katika Seneti na ingejadiliwa vilivyo. Bw. Spika wa Muda, mengi yamezungumzwa kuhusiana na utovu wa nidhamu wa Mawaziri hao kwa kupuuza kikao cha Bunge ambacho kilikuwa kimeitwa rasmi na mwongozo wa Spika ambao aliutoa wiki iliyopita. Yamezungumzwa kwamba ipo haja ya mawaziri hawa kulaumiwa kwa kukosa kuja katika kikao cha Bunge ambacho kilikuwa kimeitwa hususan kujadili kuongezeka kwa bei ya kawi ya mafuta ya petroli, taa na dizeli katika nchi yetu ya Kenya. Nimejaribu kuangalia zile kanuni ambazo zinaipa Energy and Petroleum Regulatory Authority (EPRA) uwezo wa kuamua kuongeza bei ya mafuta kila tarehe 15 ya mwezi. Nimeona kwamba kanuni hizo za kwanza zilichapishwa mnamo tarehe tatu mwezi wa kumi na mbili, 2010. Kulingana na sheria ya Statutory Instruments Act kanuni zinafaa kuwa na muhula wa miaka kumi. Inapofika miaka kumi kanuni zile huwa zinekuwa zimepitwa na wakati na haziwezi kutumika tena kama sheria katika nchi yetu. Bw. Spika wa Muda, kwa hivyo ipo haja ya Waziri atakapokuwa ameitwa rasmi kuja kueleza ni lini mara ya mwisho walipoweza kufanya ukarabati wa kanuni hizi ili ziwe zinaambatana na sheria. Jambo la pili ni kuwa KPLC imekuwa ikiritimba kwa muda wa zaidi ya nusu karne. Kwa sababu uhuru ikipatikana tulikuwa tuna shikira la East African Power and Lighting Company (EAPLC). Baadaye EAPLC ilipoondolewa tulipotoka katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikaja KPLC. Kwa muda mrefu, shirika hili lilikuwa linapata faida kubwa kwa kuuza kawi katika Kenya. Vile vile lilikuwa liko katika soko la hisa la Nairobi Securities Exchange (NSE). Bw. Spika wa Muda, ni masikitiko kuwa pesa za wale wanaostaafu katika mashirika tofauti zilikuwa pia zimewekezwa katika shirika hili. Iwapo shirika litaanguka hivyo basi wengi watapoteza rasilimali zao ambazo walikuwa wametarajia kutumia wakati wa kustaafu. Kuhusiana na swala la KPLC, ipo haja ya kuwekwa kwa tume ya uchunguzi ili kuweza kuchunguza ni kwa nini shirika hili ambalo miaka michache ya nyuma ilikuwa linapata faida kubwa kwa sasa linakuwa katika hali mahututi. Haliwezi kulipa madeni na wafanyikazi wanakataa kufanya kazi na wanafanya mgomo. Ni hali ambayo ni shirika ambalo halina mpinzani katika uuzaji wa kawi katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, tunapoangalia swala la kuongezeka kwa bei ya kawi, lazima tuangalie utendakazi wa KPLC shirika la umeme nchini. Vile vile tume ya uchunguzi iwezekupewa fursa kuangalia ni vipi ilitokea kwamba shirika ambalo halina mpinzani katika biashara, lilikuwa linapata faida kubwa kwa muda wa miaka michache limeweza kuanguka na liwe haina faida yeyote linapatikana. Kwa kumalizia, hizi kanuni ambazo zinatayarishwa na EPRA yanafaa kuwa ni mwongozo wa zile bei. Mara kwa mara lazima Waziri ashauriane na EPRA ili kuweza kuamua ni bei gani ambazo zinafaa kulipishwa wananchi. Kama ilivyotambulika ni kuwa sheria yote ama kanuni zozote ambazo zinatungwa katika nchi yetu lazina zipitie ile tunaita ushiriki wa umma ama mashauriano ya wadau."
}