GET /api/v0.1/hansard/entries/1120838/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120838,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120838/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gona",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Sen. Orengo akizumguza alitaja vifungu vingi vya Katiba lakini kuna kimoja ambacho nataka kuzungumza juu yake. Kuna kifungu ambacho kinaipa Bunge mamlaka sawa na Mahakama Kuu. Kwa hivyo, Bunge lina nguvu sawia na Mahakama Kuu. Lakini najiuliza akilini kama ni kweli Bunge ni sawa na Mahakama Kuu. Kama Bunge lingekuwa na nguvu na mamlaka sawa na Mahakama Kuu, basi wale Mawaziri wawili wangekuja jana hapa. Lakini mbona hawakuja? Ni kwa sababu kuna hitilafu ama kasoro fulani ambayo iko katika Bunge letu. Kuna baadhi ya mambo ambayo yangefanywa ile Bunge letu liwe na mamlaka na nguvu sawa na Mahakama Kuu."
}