GET /api/v0.1/hansard/entries/1120839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1120839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120839/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Gona",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Sen. Wetangula amezungumzia akasema iweje bandari tuko nayo sisi hapa Mombasa kama Wakenya lakini Sudan na Uganda wawe wanapata mafuta kwa bei ya chini na sisi tununue kwa bei ghali. Utashangaa kujua bei ya mafuta Nairobi ni afadhali kuliko Mombasa. Kwa nini basi? Kuna vitu ambazo zinafanyika ambayo sisi kama Wabunge hatuvijui. Bw. Spika wa Muda, juzi nimekuwa mazishini na watu waliniuliza kama Seneta niwaambie mbona bei ya mafuta yamepanda. Mimi sikuwa na jibu ila wale Mawaziri waje hapa watujibu maswali haya? Mimi siwezi nikamuita Mhe. Rais hapa nimuulize maswali haya. Amewateua Mawaziri ambao wanaweza kujibu maswali haya ambayo yanaambatana na maisha ya kila siku. Mafuta yanaguza mwananchi moja kwa moja. Hapo nyuma tulizungumzia masuala ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa nzige. Alitupeleka huku na kule bila suluhisho lolote. Vile vile Waziri ya Afya ambaye Wizara yake inahuzu maisha yetu. Tukasumbuka sana wakati ugonjwa huu wa korona ulipoanza kuingia tukapata shida sana na huyo Waziri. Tukaanza kumsikia sana kwa vyombo vya habari wakati ugonjwa huo uliendelea kuenea. Je, kinga na tiba afadhali nini? Hayo yote yanafanyika na Bunge bado liko hapa hapa. Bado tunasema tukisema na sisi tunabweka tu lakini hatuwezi kuuma. Jambo hili la mafuta linamguza mwananchi moja kwa moja. Hivi sasa kama alikuwa akipanda bodaboda kwenda mwendo wa shilingi hamsini, imekuwa mia au mia na hamsini ama hata mia mbili. Huyo ni yule mchochole wa chini kabisa ambaye hana kitu. Kama ni kupanda gari matatu, mahali ambapo ulikuwa ukienda kwa shilingi ishirini ama thelathini imepanda imekuwa bei ya juu. Je, tunamsaidia mwananchi ama tunamdidimiza? Hawa viongozi tuliwaeka ili waangalie mwananchi anapata afueni ama tuliwaweka wachukue lile tone la damu lilibakia walifinyange walimalize? Sasa mimi kama kama Seneta sina majibu lakini hawa Mawaziri wanamajibu ya maswali haya. Wananchi wanajua hakuchagua Waziri."
}