GET /api/v0.1/hansard/entries/1120841/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120841,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120841/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gona",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Mwananchi amechagua Maseneta, Wabunge na Mhe. Rais. Sisi ndio yule mwananchi anatuuliza maswali. Yale maswali sasa hatuwezi kuyajibu mpaka hawa mabwana. Sasa mimi pendekezo langu maanake sitakuwa mwingi wa maneno mengi yamezungumziwa, lakini nataka kugusia jambo moja. Tulizungumzia hapo nyuma tukasema misitu isikatwe maanake inaharibu maingira. Hilo nakubaliana nalo. Lakini kwa kufanya vile, tulitoa njia mwafaka nyingine kwamba wanaweza kutumia gesi, mafuta au umeme. Je, wakati huu umeme na gesi zimepanda, huyu mwananchi wa kawaida tulikuwa tumepanga apike na nini? Kama makaa kupatikana ni shida tulisema ikatizwe. Labda ile ya kutengeneza yako ghali. Saa hii ukipata mkebe mmoja wa makaa, nyinyi ni vile hampiki na makaa, mngekuwa mashahidi wangu. Makaa yako ghali sana. Watu sasa wameona njia ambayo wanawezaitumia ni njia ya kuweka umeme ili watumie gesi. Haya gesi yatumika. Watu wa umeme wenyewe wanashida. Ikiwa moto yenyewe kuipata ilikuwa wengine wanapimiwa hewa. Yaani masaa matatu mwafunguliwa na masaa mengine mshazimiwa. Kama unabiashara, una jokofu na samaki kama kule kweti wanamalizika kuoza. Hayo hayakutosha. Wapewa bili ambayo hujui ilitoka wapi. Unalipa kila mwezi---"
}