GET /api/v0.1/hansard/entries/1120846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120846,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120846/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gona",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Na Bibilia husema tawi lisilozaa likatwe. Basi Bunge la Kitaifa hawa watu mmewaweka na hawana maana na nyinyi ndio mnawahoji. Wakati umefika wa kung’ata. Tusiwe maumbwa ambao hawana meno. Sasa tuwe mbwa ambao wana meno. Tung’ate ili tumsaidie Mhe.Rais. Bw. Spika wa Muda, kama wengine walivyo zungumza hapa wamesema itawezakuwa hawa mabwana hawana makosa. Kama hawana makosa na viatu walivyo vivaa vina wafinya kupita kiasi, wavivue. Waziache hizo nafasi wachukue wengine waingie. Lakini yale ambayo yanaendelea mpaka sasa mimi namwonea huruma Mkenya jamani kwa sababu Serikali ikipandisha mafuta kila kitu kinakuwa ghali. Unga wa sima umepanda na kila kitu kimepanda. Kile cha mwananchi yule wa chini kabisa hakuna cha rahisi. Maanake kila kitu kinatumia mafuta aidha kisagwe ama kitengenezwe. Wananchi wa chini wako na afueni gani? Hakuna. Basi na wasihi tu. Kwanza nawashtumu sana hawa mabwana. Mimi ni vile sina uwezo lakini leo mngetoka maofisini maanake hamfai hata peni. Bw. Spika wa Muda, lakini kwa sababu sina uwezo, wale wenye uwezo huo basi watekeleze ili wahakikishe. Hawa wakitolewa kama hawawezi ofisi zao wakienda, itakuwa ni mfano kwa wengine ili yale ambayo tunazungumza hapa sio maneno matupu bali yawe na maana ndani yake. Kwa hayo mengi ninaunga mkono Hoja hii."
}