GET /api/v0.1/hansard/entries/1120973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1120973,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1120973/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kusimamia maswala ya elimu ya uraia. Baadhi ya pesa hizi ambazo zinatoka katika inchi za kigeni, zinatumika kuelimisha Wakenya kuhusiana na maswala la demokrasia. Kwa hivyo, ni makosa kwa Katibu huyu kuandika barua kuzuia balozi kutoa misaada. Hii ni kwa sababu misaada sio pesa pekee. Kuna misaada ya masomo na ya watu kupewa nafasi kusafiri kuenda kuangalia demokrasia nyingine zinafanya vipi. Kwa hivyo, kuzuiliwa kwa misaada hii ni pigo kubwa kwa taifa kwa sababu hatutaweza kusonga mbele kidemokrasia. Tumeona kwamba demokrasia yetu bado inayumba yumba. Hii ni kwa sababu, wakati wa kura ikifika, watu wanashikilia raho zao kwa hofu kwamba kunaweza kutokea machafuko na mambo mengineyo ambayo hayafai kufanyika. Bi. Naibu Spika, ni wazi kwamba Katibu huyu amekosa. Kwa hivyo, ile kamati ambayo itapewa fursa ya kuchunguza, inafaa imuite hapa kinagaubaga. Hii ni kwa sababu hili ni swala ambalo liahusu vyama vyote. Halihusi chama kimoja peke yake. Ninashukuru kwa sababu aliyeleta maombi haya ni Mwenye Kiti wa Wakfu was Demokrasia katika inchi ya Kenya. Kwa hivyo hili ni jambo ambalo linahusu vyama vyote kwa sababu sio chama cha Jubilee ama cha Orange Democratic Movement (ODM) ama chama cha Amani National Congress (ANC) ama Ford-Kenya ambacho kitaadhirika. Vyama vyote vimeadhirika. Bi. Naibu Spika, kwa hivyo, swala hili linafaa lichunguzwe kwa haraka kwa sababu tunaenda kupiga kura mwaka ujao tuna chini ya mwaka mmoja. Kuna mambo mengi ambayo wananchi wanatakikana kusomeshwa ili waweze kupiga kura kwa njia ya haki na usawa mnamo tarehe nane mwezi wa nane mwakani."
}