GET /api/v0.1/hansard/entries/1121237/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1121237,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121237/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ni jambo la kusikitisha hivi leo ikiwa tutaketi hapa na tutaongea jinsi vile watu wanapotea na wanauwawa na polisi. Jambo kubwa la kusikitisha ni ukisikia polisi wameenda mahali kuondoa wananchi na wako na court order, saa zingine hio court order inaeza kua ni bandia. Tena utapata ukisikia polisi wameenda mahali na wanaketi kwa muda mrefu kuondoa ni kwa sababu kuna bwenyenye, atawapa pesa na wataenda hapo kufurukisha watu ambao wapo katika mashamba yao. Watu wengine wameishi hapo kwa zaidi ya miaka sabini au themanini, maanake miti yetu inasema. Mnazi ukikua mpaka ukifa, inakua ni zaidi ya miaka sabini. Utaona polisi wako na haraka ya kwenda kushugulika na mambo ya kutesa wananchi. Wanasema wao wanaangalia ile court order inasema watu waondoke hapo. Visa kama hivi si vipya katika mkoa wa Pwani ambao umeona visa hivi kuanzia jadi. Tulikua na kiongozi katika Pwani aliyeitwa Ronald Gideon Ngala. Alikua mshupavu wa siasa na alikua wa kwanza katika Serikali yetu ya Kenya kuanzisha upande wa upinzani, yaani Kenya African Democratic Union (KADU). Hatimaye alivuma sana sababu alikua mpinzani mkubwa sana ndani ya Serikali, akipinga Hayati Jomo Kenyatta. Lakini siku moja alipatikana katika barabara ya Nairobi na Mombasa kama gari yake imependuka. Uchunguzi ulipofanywa ikawa nyuki waliingia ndani ya gari na wakauma dereva ndio ikasababisha kupenduka kwa ile gari. Visa kama hivi ambavyo Serikali haiwezi kutuambia ama kufafanua ilikuaje, ama ni ukweli kama nyuki wanaweza kuingia. Hilo tunasema si sawa. Hata hivi sasa imebainika wazi ya kwamba Mheshimiwa Ronald Ngala aliuwawa na askari. Tunajua ya kwamba kuna wanasiasa washupavu, wengine kama Mheshimiwa Karisa Maitha ambaye kifo chake mpaka hivi sasa hakijabainika uhaki wake. Imekua watu wakisema namna hii au namna ile mpaka sasa. Hawa ni watu ambao walikua wakitetea watu wa Pwani katika mashamba yao, haki zao na rasilimali zao. Bi. Spika wa Muda, jambo la kusikitisha ndani ya Serikali ilioko katika mamlaka sasa, ni kwamba wamezorotesha uchumi wa Pwani kwa sababu askari wenyewe wamekua mstari wa mbele kuzuia wale watu wanaosema hawataki ardhi yao ichukuliwe ama hawataki Standard Gauge Railway (SGR) ipitie makwao. Watu wetu wamefukuzwa katika hayo mashamba. Mashamba yamechukuliwa kwa njia si ya halali na watu wamefurushwa katika ardhi yao na hawajalipwa. Imekua sasa ni dhiki baada ya dhiki sababu polisi wanaangalia watu wasirudi tena kwa yale mashamba yao. Ukosefu wa nidhamu kama huu uliotendewa watu wa Pwani na askari ambao wanatumiwa vibaya kufurusha watu hawa katika mashamba yao ukome. Kwa sababu ukiangalia hata sasa, uchumi wa Pwani unasikitisha ajabu. Hakuna kazi, vijana wanaketi kiholela ndio sasa wanaanza kusingiziwa wamejiunga na Al Shabaab au jihad na mambo ambayo hayafai Bi. Spika wa Muda, cha muhimu ni kwamba wakati kijana ambaye anajulikana ya kwamba familia yake inamtegemea ameuwawa kinyume cha sheria au kupotezwa kinyume cha sheria, ni jambo la kusikitisha. Utaona ya kwamba wale wengi wanaopotea katika hizi sitofahamu, ni wavulana Waislamu. Si haki. Kwanini isiwe kama kuna"
}