GET /api/v0.1/hansard/entries/1121241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121241,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121241/?format=api",
    "text_counter": 377,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": ", ilikua na ripoti nzuri sana. Ilieleza chanzo cha polisi kutumia nguvu, chanzo cha watu wa Pwani kupoteza mashamba yao na chanzo cha vile mashamba yalinyakuliwa. Hili jopo liliandika ripoti. Bi. Spika wa Muda, ni miaka mingi sana, zaidi ya miaka kumi sasa tokea hii ripoti ya Truth and Justice Reconciliation Committee ambayo ni Ukweli na Sheria na Uridhiano, na haijatolewa mpaka hivi leo. Ripoti hii ilikua hususan inaongea mambo ya Pwani. Watu ambao waliweza kupata uhuru tokea kitambo lakini watu wa Pwani hawakupata uhuru wao mpaka mwisho ikifikia mwaka wa elfu moja mia tisa sitini na tatu; Kenya ikipata uhuru, maeneo ya Pwani yalitengwa. Yalikua si mojawapo katika Pwani. Mwaka wa 1964 Kenya ilipokuwa imepata uhuru sasa na kuwa Jamhuri, ndio Pwani ikakaribishwa. Ilipokaribishwa iliambiwa kwamba mtu wa Pwani yeyote akiwa na haja ya kupata ardhi ndani ya Pwani, ilikuwa ni sharti apate sahihi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya. Sasa tunauliza maswali kwamba je, watu wangapi walikuwa wanaweza kumfikia Rais na kumwambia hapa tunapoishi tunafaa kupewa ardhi? Bi Spika wa Muda, ripoti hiyo ya Kamati ya Haki, Maswala ya Kisheria na Haki za Binadamu iweze kuweka wazi ile Ripoti ya Truth Justice and ReconciliationCommission (TJRC). Iweze kuwekwa wazi, Wakenya waisome na watu wa Pwani pia waisome. Wajue ni kitu gani kimeandikwa pale isije ikawa na msemo tu kila mwaka. Mwaka nenda mwaka rudi tunasema fungueni hii Ripoti na mpaka leo haijafunguliwa. Naunga mkono sana haya mapendekezo yamefanywa kwamba hii Ripoti iweze kuangalia na lile jopo la Independent Policing Oversight Authority (IPOA) iwezekuchunguza polisi ambao wanawaua watu kiholela na kuangamiza watu kiholela. Naunga mkono pendekezo hilo liweze kupewa kipau mbele. Bi Spika wa Muda, nikisema hivo, huko nyumbani kuna jambo la kusikitisha. Kuna kijana mmoja kwa jina Mohamed ambaye aliyekuwa na miaka 16. Ilikuwa tarehe 22 Septemba, 2017. Aliondoka nyumbani akiwa ametumwa na familia yake kwenda tu kununua maziwa dukani, na hakurudi tena nyumbani. Mpaka hivi leo, wazazi wanalia wanataka haki zao na kijana hajaonekana mpaka leo. Kuna kijana mmoja pia kwa jina maarufu “Major.” Alikuwa na rafiki yake wa dhati. Baada ya kumpeleka uwanja wa ndege - alikuwa anaondoka akienda nje ya nchi - kijana huyu hajarudi nyumbani mpaka leo, na hajaonekana. Bi Spika wa Muda, vile vile, kuna majirani kama mzee mmoja kwa jina Abdi Farah. Alikuwa na mtoto wake kwa jina Mohamed. Mtoto wake alikuwa anaenda shule ya upili. Mpaka leo huyo mtoto hajarudi nyumbani. Imefika mwaka wa tatu sasa. Pia"
}