GET /api/v0.1/hansard/entries/1121243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1121243,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121243/?format=api",
"text_counter": 379,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "kuna mtu mzima mmoja kwa jina Mzee Abubakar. Alisingiziwa kuwa yeye ni jambazi. Hatimaye aliweza kuwekwa ndani. Badala ya kupelekwa polisi, sasa amepotea na hatujui aliko. Vile vile, hatuwezi kusahau. Kuna watu ambao wamepitia mkono wa polisi ambao hawakupelekwa kortini. Ukiangalia kule nyumbani, kama Mombasa, kuna mwalimu wa dini kwa jina Makaburi. Aliambiwa kwamba anafundisha watoto jinsia mbaya. Lakini hakuna hata siku moja tuliona Makaburi amepelekwa kortini na akaambiwa hivi ndivyo alivyo fanya na kwamba sio haki na akafungwa. Bi Spika wa Muda, bali tuliona Makaburi akipigwa risasi. Alikuwa ameshatabiri kwamba polisi wanamtafuta na watamuua. Mpaka leo, baada ya kusema hivyo, hajukatokea jawabu lolote. Familia yake inalia mpaka leo wakisema wanadai haki yao. Kuna mtu mkubwa sana aliyekuwa mheshimiwa kwa mambo ya dini. Alikuwa anaitwa Muhamed Abdi Rogo. Rogo alikuwa mwalimu ambaye alikuwa anahusika sana na mambo ya kufundisha watoto na watu wazima. Alikuwa ni mkubwa wa misikiti ya kiislamu katika Pwani. Ni mtu alikuwa anaheshimika sana. Alipigwa risasi akiwa na bibi na mtoto wake ndani ya gari. Bibi na mtoto wakawachwa na hao polisi. Bi Spika wa Muda, tunauliza: Ikiwa watu kama Makaburi na Abud Rogo wanaweza kuuawa na ni mwalimu wa dini ambaye alikuwa anajulikana sana, kwa nini wasishikwe wapelekwe kortini alafu washatakiwe na tuone haki ikitendeka wakati korti inatoa uamuzi? Ni makosa sana kwa askari kushika watu na kuwapoteza. Mpaka hivi sasa, familia za Makaburi na Abud Rogo, ambaye alikuwa anaketi katika kaunti yangu ndani ya Kikambala--- Alikuwa anaishi kama jirani yangu pale Mtwapa. Alipigwa risasi na haki haijatendeka mpaka sasa. Bi Spika wa Muda, naunga mkono Ripoti hii na kusema kwamba hatua ichukuliwe na hata hawa askari ambao wako na tabia kama hizo ambazo wanazifanya za kupoteza watu, kitengi cha sheria kichukue mkondo wake. Asante."
}