GET /api/v0.1/hansard/entries/1121245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121245,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121245/?format=api",
    "text_counter": 381,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ripoti ya Kamati ya Haki, Maswala ya Kisheria na Haki za Binadamu ya Seneti kuhusiana na swala la mauaji ya kiholela ya polisi. Hiyo ni pamoja na kupotezwa kwa Wakenya wengi ambao wanaendelea kupotea kila siku kupitia kwa vitengo vya polisi. Kutoka Seneti hii ianze kazi mnamo Mwezi wa Tisa, 2017 kumekuja Taarifa takriban 20 zinazungumzia maswala ya watu kuuliwa kiholela na polisi pamoja na wale ambao wanapotezwa na polisi hao. Bi Spika wa Muda, hata hivi sasa tunavyo zungumza, watu wanaendelea kupotezwa na wengine wanachukuliwa. Kwa mfano, Abdul Hakim Sagar alichukuliwa Mombasa Tarehe 18 Agosti mwaka huu. Kwa bahati nzuri, akaachiliwa baada ya mwezi mmoja msituni karibu na mji wa Voi. Mwingine aliyechukuliwa katika visa kama hivi ni Prof. Abduswamad ambaye alichukuliwa mwezi huo wa Agosti na akakaa ndani kwa muda wa wiki tatu. Baadaye akaachiliwa hapa Nairobi bila mashataka yeyote na akaonywa kwamba asizungumzie swala hilo la kutekwa kwake."
}