GET /api/v0.1/hansard/entries/1121247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121247,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121247/?format=api",
    "text_counter": 383,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi Spika wa Muda, mwingine ambaye amechukuliwa ni kijana anayeitwa Muhamed Abubakar Said ambaye alitekwa nyara mnamo tarehe 14 Oktoba mwaka huu maeneo ya Mombasa karibu na Msikiti wa Musa. Mpaka leo, hajulikani yuko wapi. Mwingine aliyechukuliwa ni Prof. Hassan Nandwa ambaye alichukuliwa tarehe 18 mwezi huu na akachiliwa jana maeneo ya Makueni, mahali ambako alikuwa hajulikani. Kwa hivyo, ni visa ambavyo vinaendelea kila siku. Juzi nilifurahi kwamba mahakama ilitoa amri mpaka zile kumbukumbu za simu zile za Safaricom waliombwa wazilete mahakamani kuonesha vipi mwelekeo wake kutoka alipochukuliwa mpaka pale alipokuwa amefikishwa. Mnamo mwezi wa Nne nafikiri mwaka wa 2019, nilileta Taarifa pia hapa Bungeni ya kijana anayeitwa Husni Mubarak ambaye pia alipotezwa. Kutoka wakati huo mpaka sasa bado hajulikani alipo. Bi Spika wa Muda, hatupingi vita dhidi ya ugaidi, lakini tunasema kwamba kila kitu lazima kifwate sheria. Nchi yetu inalindwa na sheria na ina Katiba ambayo sote tuliipigia kura mnamo mwaka wa 2010. Nchi haina shida ya sheria. Mahakama zetu zinafanya kazi. Ijapo kuwa nitalizungumzia mbeleni kidogo, kwa sasa tunaweza kusema kwamba mahakama zinaweza kufanya kazi ya kuamua kesi yeyote ambayo inawezakuwa dhidi ya mtu yeyote katika nchi yetu ya Kenya. Bi Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha kwamba bado mpaka sasa tunapata visa kama hivi ambavyo vinaendeshwa na polisi pamoja na vyombo vingine vya serikali. Hakuna mtu anaweza kuvamia mtu na bunduki mchana na wako karibu sita au saba, wote wako na bunduki na magari ambayo hayana nambari za usajili, wakamshika mtu na wasimpeleke mahakamani ispokuwa ni polisi. Niliwahi kuenda na chama cha Haki Africa mpaka kwa ofisi ya Director of Public Prosecutions (DPP) na tukalijadili swala hili kwa kirefu. Lakini DPP akawa hayuko tayari kutoa habari zozote kuhusiana na swala hili. Bi Spika wa Muda, ripoti hii imekuja wakati mzuri sana kwa sababu nchi bado ina matatizo haya ya watu kuuliwa na kupotezwa kiholela. Swala hili limekuja wakati huu wa serikali ya Jubilee. Hii miaka tisa ya serikali ya Jubilee ndiyo imeleta matatizo haya ya enforced disappearances. Ndugu Sen. Madzayo amezungumzia kuuliwa kwa Sheik Abud Rogo, Makaburi na wengi ambao wanauliwa na hatuwezi kuwataja hapa. Kuna vijana wengi ambao walichukuliwa kutoka Kwale wakaenda kuuliwa Tsavo na mili yao ikatupwa kule mpaka ikaharibika. Juzi watu wa Haki Africa walipata mili kadhaa sehemu za Tana River ambapo watu walikuwa wameuliwa kwa njia ambazo sio sawa. Mili yao ilionyesha kwamba waliteswa kabla ya kuawa. Bi Spika wa Muda, haiwezekani kwamba serikali iwe ina wadhulumu raia wake kiasi kama hiki. Hivi visa vya watu kupotezwa katika Lamu ni vingi sana. Sehemu kama Kaunti ya Lamu, hakuna sheria ya utangamano kule. Kila siku jioni ikifika saa kumi na mbili unaambiwa sasa hii ni eneo la operesheni na magari ya raia hayaendi, lakini magari ya kubeba vitu kama miraa na bangi yanakwenda masaa 24 bila shida yeyote. Sehemu kama Lamu inafaa iangaziwe zaidi kwa sababu kule kuna visa vya kila siku vya watu kupotezwa na wengine kuuliwa bila kutumika kwa sheria yeyote. Bi Spika wa Muda, mahakama yetu kwa sasa imelegeza kamba kuhusiana na maswala haya. Zamani ilikuwa ukiripoti kwamba mtu amepotea au ameshikwa na polisi kwa njia ambayo sio sawa na hajapelekwa Mahakamani, ukitoa ombi ile inaitwa kwa"
}