GET /api/v0.1/hansard/entries/1121249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121249/?format=api",
    "text_counter": 385,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kiingereza habeas corpus, polisi walikuwa wanapewa masaa 24 kumleta mhusika kortini ama wamuachilie. Lakini sasa mahakama inaweza kutoa amri kwamba aje baada ya siku saba. Kwanza ukipeleka kwa cheti cha dharura, watakuambia kwamba nenda ukapeleke makaratasi kwa Mwanasheria Mkuu ama kwa DPP. Yakipelekwa kwa DPP, akija kortini anasema: “Sijapata maelezo kutoka kwa Inspector General of Police (IG), nipe siku saba, kumi au 23.” Ni njia ya kuaihirisha kesi wakati swala la haki za kibinadamu ni la dharura. Lazima hatua ichukuliwe pale pale. Sheria inawapa polisi masaa 24 kumshika mtu. Ikizidi zaidi ya hapo ni jambo la dharura. Kwa hivyo ni lazima watu waweze kuelezwa mtu yule anashikwa kwa sababu gani. Bi Spika wa Muda, nataka kuwapatia mfano amboa uko hai kabisa. Wakili Willie Kimani aliuliwa mwaka 2017 kama sijakosea. Wakati ule bado nilikuwa nafanya kazi ya uwakili. Hata tukavaa zile pink ribbons kuomboleza dhulma aliyofanyiwa kijana huyo. Mwili wake ulipatikana ndani ya gunia. Unyama ulioje? Uuwe mtu alafu umtie ndani ya gunia na utie gunia kwenye mto ili asiweze kupatikana kabisa. Kesi ya Willie Kimani mpaka sasa ipo mahakamani. Lakini George Floyd ambaye aliuliwa kule Amerika alipozuiliwa pumzi akafariki kule mwaka wa 2020 mwezi wa Mei. Kesi yake imeskizwa na ikamalizika na yule mtu ambaye alimuuwa akafungwa miaka 22 mwezi wa Septemba mwaka huu. Kesi ya Willie Kimani bado iko mahakamani. Ni jambo la aibu mahakama zetu zina shindwa kuamua mambo ya haki za kibinadamu wakati watu wana lalamika kuhusiana na haki hizo katika nchi yetu ya Kenya. Bi Spika wa Muda, utapata kwamba kesi zote ambazo zinatokea za watu kupotezwa, walio na ushahidi ni polisi pekee yake. Kwa nini kama wana ushahidi kwamba huyu ni mhalifu hawawezi kumfikisha mahakamani wakasema kwamba sisi tuna ushahidi huu. Tunataka kumzuia huyu kwa siku kadhaa ambapo tufanye uchunguzi zaidi ili familia ijue kwamba mtu wetu yuko mahali gani na anazuiliwa kwa sababu gani. Ukiangalia wazazi wengi ambao wamepatikana na swala kama hili kwa kupoteza watoto wao, wengi wanashindwa hata kula. Nita kupa mfano wa mzazi wa Muhamed Abubakar Saeed. Mamake mpaka sasa amesusia chakula kwa muda wa siku 14. Leo ni zaidi ya wiki tatu kijana huyo hajapatikana na tunajua ni polisi na vyombo vya dola ndizo vimeweza kumshika na kumpeleka mahali ambapo hapa julikani. Bi Spika wa Muda, kabla ya mapendekezo ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa kamati kwa kuzuru mji wa Mombasa ambapo visa vingi kama hivi vimeweza kutotea. Nachukua fursa hii pia kutoa shukrani za dhati kwa Mombasa Law Society kwa kujitokeza kuzungumzia swala hili, Haki Afrika, Shirika la Muhuri, Shirika la Huria na mashirika mengine yote ya pwani ambayo yaliweza kujitokeza siku ile Seneti ilienda Mombasa kwa vikao vya kuwaskiza wananchi. Tukija kwenye mapendekezo, nakubaliana hususan na mapendekezo yote ambayo yametolewa katika swala hili. Tukiangalia mambo mengi yanato kana na uzembe wa serikali. Kwa mfano, kuratibiwa kwa sheria ya Coroners Act ambayo imepitishwa zaidi ya miaka miwili iliyopita, hilo ni swala ambalo Mwanasheria Mkuu inafa aje Bungeni aeleze ni kwa sababu gani haija tekelezwa sheria hii. Ingeweza kuwapa fursa madaktari kutoa ushahidi wa kina kuhusiana na lini kitu gani ambacho kime sababisha kupoteza kwa maisha ya mtu."
}