GET /api/v0.1/hansard/entries/1121251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121251/?format=api",
    "text_counter": 387,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi Spika wa Muda, kuna ulinzi wa mashahidi. Kuna watu karibu watatu ambao walichukuliwa kama mashahidi wakati wa vita vya Al-Shabaab. Wote baada ya muda wakaondolewa ulinzi wao na wote wakauliwa. Mmoja alichinjwa katika sehemu ya Marafa kule Malindi. Ipo haja ya kuongeza ufadhili wa ulinzi wa mshahidi. Bila ya kuwalinda mashahidi, kesi nyingi hususan za polisi zitaweza kupotea bila kuwa na mwelekeo wowote. Kitu kingine ambacho ningeweza kuipongeza kamati ni pendekezo lao la kuwa na msaada wa kisaikolojia kwa wale ambao wame athiriwa. Kuna wazazi ambao kwa Kiingerea tunawita “single parents” ambao labda mtoto wake mmoja pekee yake ndiye amepotea na hajulikani aliko. Mwaka jana kule sehemu za Diani, polisi walivamia mji wakampiga risasi baba na watoto wake wawili. Mama mmoja pia akapigwa risasi ikabidi aende akazae hospitalini. Maswala kama haya wanataka kufanyiwa ushauri ili waweze kuwa na imani kwamba yaliyotokea hayawezi kutokea tena kwa siku za usoni. Bi Spika wa Muda, swala la Independent Policing Oversight Authority (IPOA) kuongezewa ufadhili ni muhimu sana. Hii ni kwa sababu IPOA mpaka sasa haina ofisi katika kila kaunti katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ni shirika ambalo linafanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba zile dhulma zinazo fanywa na polisi zina chunguzwa na wale wanao husika wanapewa adhabu. Ipo haja ya serikali kuongeza ufadhili kwa IPOA ili kuona kwamba zile kesi zina chunguzwa kwa haraka na wale wahusika wana shtakiwa mahakamani bila shida yeyote. Tunasema pia Kenya National Human Rights Commission (KNHRC), makamishna kule pia wamezembea katika kazi zao. Wamelala wakati Wakenya wanalalamika juu ya visa kama hivi. Mwaka jana tuliweza kuhudhuria hafla ya Haki Africa ambapo walikuwa wanatoa ripoti yao kuhusiana na mauwaji ya kiholela wakati wa janga la virusi vya Korona. Ilikuwa ni ripoti ya kusikitisha. Bi Spika wa Muda, wiki iliyokwisha nilihudhuria warsha ya Independent Medico- Legal Unit (IMLU). Walisema kwamba mpaka sasa kwa mwaka huu pekee yake zaidi ya watu 30 washauliwa katika njia za kiholela kutokana na vitendo vya polisi."
}