GET /api/v0.1/hansard/entries/1121625/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1121625,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121625/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Ni vyema kuangalia kwa kina mambo ya ardhi. Kuna desturi ya Wabunge wengine, sisemi wote, zaidi wa Miji Kenda, ikifika wakati wa uchaguzi, lao kubwa wanataka kuona ardhi gani inamilikiwa na Bajuni au Muarabu ili watume watu waingie hapo au wasaidie kuzuia court order . Hawana shida na watu wa bara wakimiliki ardhi. Lakini siasa zao siku zote ukiangalia ni hizo nilizotaja. Huu ni uhasidi. Miji Kenda wanakaa sehemu zingine. Lamu tuna Miji Kenda. Tunawaheshimu na wana ardhi. Ni haki yao wawe nazo kwa sababu ni Wakenya. Lakini badala ya wao kuonyesha maendeleo wamefanya kwa miaka mitano, mambo yao ni kusimama kwa majukwaa. Haki ya Mungu nenda ukaangalie saa hii. Miji Kenda wanapeleka watu wavamie ardhi."
}