GET /api/v0.1/hansard/entries/1121816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121816,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121816/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Mhe. Didmus Barasa kwa Mswada huu mzuri wa pesa za uzeeni. Kwa hakika, inapofika siku ya mfanyikazi kustaafu, tumbo huwa linakataa kustaafu. Linataka kula kila siku. Pesa hizo zikichelewa kufika, yule mfanyikazi atakula nini? Tunajua kuwa watu wetu wakipata pesa, wanazitumia wakijua kuwa kuna pensheni yao ambayo itawasaidia kule mbele. Kwa hivyo pesa hizo zikichelewa, jambo hilo linamuumiza yule mfanyikazi na anachukua madeni. Hata hiyo pensheni ikifika, haitumii kwa njia nzuri. Wale ambao wanachukua pensheni yao wanatoka sehemu mbali mbali kwa mfano, Kiunga, Mkokoni na Tiwayu. Pengine hamjui kule ninakotaja. Ni kule kwenye hiyo pembetatu. Chifu wa huko atakuja Nairobi na kuzunguka kwa maofisi akiambiwa mara barua hii haipo, akaunti hiyo haifai na kadhalika. Atarudi Lamu na kuambiwa kuwa benki hii haifai kwa hivyo afungue akaunti nyingine. Yule Chifu atatumia Ksh2,000 kutoka pale Kiunga mpaka Lamu. Hizo ni pesa za safari ya kuja peke yake, bado hajarudi. Tena, hakuna usafiri wa kila siku. Akitaka kufanya mambo kwa haraka ili aende siku ambayo boti haijafika, itabidi akomboe boti kwa Ksh30,000. Tukisema kuwa kule kwetu kuna shida, watu wanaona ni kama tunataka kulia tu. Njia za usafiri ni ngumu. Vitengo vingi vimekuwa vikipata matatizo. Mojawapo ni wale wanaofuatilia pesa zao za uzeeni. Tunapaswa tuwakuze wenye kutoa ile pensheni. Tusiwe tu tunalalamika. Sisi hapa tuna jukumu la kuwawezesha. Kwa mfano, kaunti zinakata pesa za uzeeni lakini hazipeleki pesa hizo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}