GET /api/v0.1/hansard/entries/1121817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121817,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121817/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "kwa wale wa kuwekeza mfuko wa pesa za uzeeni. Ni mbinu gani tutatumia kuhakikisha kuwa pesa hizo zinafika kule? Pia wao wanatatizika. Hawataki kukosa kulipa pesa za uzeeni lakini hawapewi pesa hizo. Sisi hapa katika Bunge tunafaa kuhakikisha kuwa tumeweka sheria ili pesa za uzeeni za kaunti zikatwe na kupelekwa kwa wawekezaji kabla hazijawafikia ndio waweze kulipa kwa muda unaostahilika. Tusiweke tu sheria. Naunga mkono sheria hii. Ni sheria nzuri na ninajua itasaidia. Lakini hii sheria ikiwepo, tutatafuta mikakati ya kuwasaidia wale wanaotoa zile pesa za uzeeni. Kusema ukweli, hata pensheni ya Serikali huchelewa sana lakini nawapongeza pia kwa ile kazi wanaofanya. Tunapaswa kuchukua jukumu tukae nao, tusikize matatizo yao ili tujue ni kwa nini wanafanya hivyo. Tusipitishe sheria tu. Huwa tunapitisha sheria zingine kisha hatufuatilizi kujua kuna mikakati gani ya kuzitekeleza. Kwa mfano, tulitunga sheria hapa kuhusu uvuvi na imebidi nimepambana kule Lamu. Sheria iliwekwa tu lakini hawakuenda kuangalia ni mbinu gani ile sheria itasaidia yule mvuvi. Naogopea hivyo kuhusu sheria hii. Ni kweli wazee wetu wanateseka lakini namuomba Mhe. Didmus Barasa atumie kamati ili ije hapa itueleze kwa nini wanafanya hivyo. Itueleze pia ile mikakati itaweka kuhakikisha kuwa ndani ya siku 90, wawe washalipwa baada ya kupitisha sheria hii. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Sina mengi zaidi."
}