GET /api/v0.1/hansard/entries/1121835/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121835,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121835/?format=api",
    "text_counter": 251,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "ama kundi fulani ambalo linatumia ufisadi katika mambo ya pensheni . Imekuwa kwamba mpaka uhongane ama utoe pesa kadhaa ndiposa uweze kupata pensheni yako kwa wakati unaofaa. Ndugu yangu Didmus amependekeza siku 60 ambazo ni mwafaka kabisa kwa aliyestaafu aweze kupata pesa za pensheni . Tukiangalia changamoto zinazofanya hizi scheme za pensheni kuwa na matatizo, mara nyingi sana tunapata ule uwekezaji wanafanya ni duni ambao hauleti mapato. Suala jingine ni usimamizi wa hii pensheni. Kuna usimamizi mbaya, ikiwemo ufisadi. Hivyo basi, inakuwa changamoto kupata pesa za kulipa watu pensheni. Pia, kuna waajiri wengine ambao wanakuwa muflis, ama bankrupt . Mtu anakosa pesa na anakuwa muflis, hivyo basi wale watu anafaa kuwalipa pensheni wanapitia ugumu sana. Wazee wengi wamehangaika. Wengi wamekufa na huzuni. Wengi wameshikwa na maradhi sugu kwa sababu ya kukosa pensheni ambayo ingewawezesha kuishi yale maisha waliokuwa wakiishi wakiwa wameajiriwa. Hivyo basi, lazima Wizara ya Fedha iweze kuweka mikakati kambambe ambayo itawezesha mawasiliano kati ya muajiriwa na muajiri kuhusu mambo ya pensheni. Watu wengi pia hawaelewi ni wakati gani wanaweza kupata pesa za pensheni ama njia ya kufuata kuzipata. Pia, kumekuwa na urasimu mwingi. Kwa Kiingereza, urasimu ni bureaucracy . Watu wengi wanashindwa kufuatilia urasimu kama huo ili wapate pesa za pensheni. Lazima tuige kutoka nchi nyingi zilizostawi. Nchi hizo huwa wameweka bima ambayo itawezesha muajiri, akiwa na changamoto za kifedha, kuweza kulipa pensheni. Hata kwa muajiri ambaye amekuwa muflis, atafaidika na bima ile kulipa watu pensheni kwa wakati unaofaa. Tuna mashirika katika Serikali yetu, kwa mfano katika vikosi vya jeshi na polisi, iwapo afisa amefariki akiwa kazini, mjane anapata shida sana kufuatilia pensheni iweze kusaidia wale watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kisheria wa miaka 18. Kwa hivyo, ni lazima hii mikakati iwekwe katika kila sekta ya umma na za kibinafsi ili tusiwe na tashwishi yoyote katika mipango hii. Kwanza kabisa, zile pesa muajiriwa anafaa kulipa, kama za NSSF na NHIF, ni muhimu sana muajiri alipe kwa wakati unaofaa. Nyakati nyingi unapata muajiri ako na changamoto kulipa pensheni kwa sababu anakosa kulipa zile pesa za lazima. Hii tunaona sana katika sekta ya umma, haswa katika serikali za kaunti. Kaunti nyingi ziko na changamoto kulipa pesa hizi za lazima ambazo zinawezesha waliostaafu kupata pensheni yao kwa wakati unaofaa ili wasaidike. Sasa hivi, tuna changamoto ya maradhi sugu kama maradhi ya kisukari, saratani na korona. Je, katika hizi skimi za pensheni tumeangazia mambo ya afya? Wakenya wengi ambao wamestaafu wanapata changamoto ya afya na elimu kwa wtaoto na familia yao. Haya ni mambo ambayo lazima yapigwe msasa na sera muafaka ziwekwe na kuambatanishwa na Mswada huu. Tunapopitisha Mswada huu, tujue kwamba ni sera, mikakati, au ni sheria gani zitakuwa sawia kuhakikisha kwamba Wakenya wengi hawatalia tena. Wakenya wengi wamepoteza maisha, wengine wakiamua kujitoa uhai kwa sababu ya kukimbizana wakitafuta pesa zao za pensheni. Imekuwa ni kana kwamba ni paka mshike panya. Unakwenda ofisi kwa ofisi. Ukitoka ofisi hii unaambiwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}