GET /api/v0.1/hansard/entries/1121836/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121836,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121836/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "upitie ofisi nyingine. Ukitoka huko, unaambiwa utengeze barua fulani. Ukimaliza hii, unatengeza hii. Yaani ni urasimu mwingi. Nashukuru sana ndugu yangu Mhe. Didmus Barasa. Mambo haya ya uwekezaji wa pesa za pensheni lazima yaangaziwe kitaifa. Iwapo kuna utaratibu wa pensheni lakini inazembea na inaonekana sio ya kusaidia Wakenya walioko humo, lazima Serikali iwe na njia ya kuwaadhibu wasimimamizi wale kwa kosa kama hilo. Mkenya hawezi kuwekeza pesa zake akijua muajiri atawekeza zaidi ili mapato yakija aweze kurudishiwa zile pesa za pensheni, lakini kumbe pesa zile zinatumika kwa kiholela na tunakuwa na changamoto sana katika mambo ya pensheni. Familia nyingi zimeathirika sana na kuporomoka kimaisha. Watu wengi wanalia. Watu wengi wamepoteza uhai wao bila hata kupata pensheni zao. Mbali na pensheni, ndugu yangu amezungumzia malumbikizi ama gratuity . Fedha hizi pia zimekuwa na changamoto. Unaambiwa ukimaliza kandarasi ya uajiri kwa muda fulani, utapata pesa hizo. Lakini unamaliza kandarasi ile na unakaa kwa muda mrefu sana bila kulipwa pesa zile. Pengine mtu amepangia peza zile. Mambo kama haya lazima tuyafuatilie kwa kina kama Wabunge, haswa kwa utekelezaji."
}