GET /api/v0.1/hansard/entries/1121849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121849,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121849/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": {
        "id": 13287,
        "legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
        "slug": "kassim-sawa-tandaza"
    },
    "content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Mshwada huu wa pesa za wanaostaafu. Ni kawaida, na huwa ni furaha wakati mtu ameweza kufanya kazi mpaka akastaafu. Maanake ni katikati huwa kuna changamoto nyingi sana. Lakini, wakati mtu ameweza kufanya kazi, kwa dhaatima na heshima na familia yake mpaka akastaafu, kwanza, ni kumshukuru Mwenyezi Mungu. Lakini, changamoto inayokuja ya kuwa hajui ataanzia wapi, ni jambo la kuhuzunisha na ni linachangia katika maswala ya ufisadi. Na ndio maana naunga mkono Mshwada huu ikiwa mimi ni mmoja wa wale huwa nakemea sana swala la ufisadi na kuona ni vipi tunaweza kulipunguza swala hili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}