GET /api/v0.1/hansard/entries/1121850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121850,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121850/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": {
        "id": 13287,
        "legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
        "slug": "kassim-sawa-tandaza"
    },
    "content": "Mtu akifanya kazi anapokea mshahara wake wa halali lakini anajua kwamba atastaafu na inamaanisha kuwa hataweza kupata tena ule mshahara. Hataweza kupata ile ruzuku yake. Inamaanisha aanze kufikiria njia mbadala ya vile ataweza ishi atakapostaafu. Kama tunavyojua, njia mbadala mara nyinyi ukiwa kazini na unapenda kazi yako, basi, watu husema kuwa mtu hula pale pale anapofanyia kazi. Lakini, sio kukula tu, na ndio maana watu wanaanza kufikiria ni vipi wataweza kupora mali, waweza kujijenga mbali na lile pato lao la kawaida. Hii sio siri maana waajiri wa Serikali wanajua. Kwa hivyo, kuwapatia wafanyikazi njia ya kuwa na uhakika wa kuwa hata wakistaafu, bado ile haki yao wataweza kuipata moja kwa moja, ni njia moja ya kupunguza ufisadi katika ofisi zetu za umma na hata za kibinafsi. Pili, katika swala hili nyeti, nishawahi kufwatwa na wafanyikazi ambao Mwenyezi Mungu ameweza kuwabariki na umri mrefu. Kuna wale ambao walifanya kazi nyakati za East AfricanCommunity, ambapo, hususan, walikuwa katika ile idara ya uchukuzi iliyoitwa Kenya CargoHandling kabla iwe Customs na baadae kujumuishwa katika maswala ya utoaji ushuru. La kustaajabisha ni kwamba wale waliofanya kazi nyakati hizo mpaka sasa hawajapata ruzuku zao ilhali walifanya kazi kihalali na kwa moyo moja. La kuhuzunisha ni kuwa wanakuambia hili ni kwa sababu wakati ule walikuwa waariwa wa Kenya lakini idara ikapelekwa Dodoma ama nchi nyingine katika ile iliyokuwa Jumuiya ya Mashariki ya Kati. Wenzao walilipwa kwa wakati ambao unafaa kwa sababu ni watu ambao bado wako hai na wanawasiliana. Lakini, Wakenya waliokuwa Kenya, mpaka sasa bado hawajalipwa. Swala hili la siku tisini ijapokuwa sheria huwa haiendi nyuma kuanzia pale ulipowekwa kidole, ni maombi yangu kwamba sheria hii tutakapoipitisha hapa Bungeni, kwa sababu wengi tunaiunga mkono kutokana na wale waliotangulia kuzungumza, tuweze kuangazia maswala ya wale waliostaafu kabla ya hii sheria kupitishwa na mpaka sasa bado hawajapata haki yao ili nao waweze kuangaliwa. Ninafikiri itakaposomwa kwa Mara ya Tatu, hayo ni baadhi ya maswali ambayo yanaweza kuongezwa katika vipengele kuona kwamba watu hao wanaweza kupata ruzuku zao. Katika maswala hayo ya pensheni, kulingana na Mswada huu wa Mhe. Barasa ambaye nampea kongole kwa kufikiria na kuufikisha kwenye Bunge hili, ni lazima pia kuwekwe vikwazo kuhusu hatua itakayochukuliwa kwa muajiri ambaye atakiuka sharia hii, hususan Serikali, kwa sababu ni lazima tukubali kwamba katika maswala haya yote ya pensheni, Serikali ndio hugeuka hizi haki za wafanyaji kazi.Ikiwa baada ya siku tisini mtu hajapata marupurupu au hajalipwa pensheni yake, ni hatua gani itachukuliwa? Katika kuweka sheria, ninafikiri ni bora tuongeze vikwazo wakati wa kuisoma tena. Hii ni kuhakikisha kuwa mtu anashurutishwa. Kwa mfano, wakati mtu atakuja na aambiwe kuwa kitambulisho au picha yake haionekani. Nimepata wazee ambao wanasema wamepata vikwazo kama hivyo ya kwamba wanapeleka kila kitu lakini wanaambiwa kuwa vitambulisho au picha zao zikiangaliwa hazionyeshi ni wao ambao wanadai zile pesa. Vikwazo hivi havina maana. Hivyo basi, muajiri anapojua kuwa asipolipa katika zile siku zinazohitajika, atahitajika kulipa mara mbili ya vile ambavyo angehitajika kulipa, basi kutakuwa na ushirikiano. Hii ni kwa sababu kutakuwa na majukumu mawili. Yule mwenye kutaka pensheni yake anazitaka kwa sababu ya mahitaji yake na muajiri anataka alipe kwa sababu asipolipa kutakuwa na penati fulani. Yeye pia atapata hasara kutokana na kutolipa. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, katika suala hili, kawaida mimi huunga tu mkono. Ningependa kuongezea kwamba katika Mswada huu sitaunga tu mkono, bali pia miguu kwa sababu kuna watu wengi kule kwangu Matuga ambao wananipatia gharama kubwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}