GET /api/v0.1/hansard/entries/1121851/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121851,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121851/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": {
        "id": 13287,
        "legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
        "slug": "kassim-sawa-tandaza"
    },
    "content": "Nikiongezea, katika hii idara ya kulipa pensheni, ingawa sio lazima iwe kwa sharia, ningeomba pia wapatiwe sindikizi ya kuona kuwa ofisi hizi zinasambazwa mashinani. Hii ni kwa sababu changamoto iliyo ni kwamba yeyote ambaye atahitaji kulipwa marupurupu yake ni lazima aje Nairobi. Ile gharama ya kuja Nairobi kwa mtu ambaye alistaafu ni kuu. Ukweli ni kwamba wapo ambao mwenyezi Mungu amewajalia kustaafu wakati mshahara wao ulikuwa chini ya Kshu10,000. Sasa hivi, umepanda hadi ni zaidi ya Ksh100,000. Ikiwa wakati ule alipostaafu mshahara wake ulikuwa ni chini ya Ksh10,000, inamaanisha kuwa pensheni yake haifiki Ksh2,000. Lakini pia yeye analazimika kusafiri kuja Nairobi kutafuta haki yake. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba hiyo ofisi ya pensheni inayohusika ina ofisi kule nyanjani pengine katika hizi Huduma Centres ili zishughulikie masuala kama haya na kuyafikisha mwisho na sio tu kuchukua stakabadhi labda na kuzituma Nairobi na kisha baadaye watu wanaambiwa kama wenzangu walivyotanguliza kuwa faili ilipotea, next of kin bado haonekani au kitambulisho kina vikwazo vidogo vidogo. Kwa hivyo, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu na nikimalizia, sio tu mkono lakini pia na miguu na itekelezwe haraka iwezekanavyo. Asante sana."
}