GET /api/v0.1/hansard/entries/1121999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1121999,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1121999/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kumaliza mchango wangu kwa ripoti hii. Niliposimama jana, nilikuwa nimeeleza kuwa baadhi ya wale ambao walichukuliwa na hadi leo hawajapatikana ni kijana anayejulikana kwa jina la Mubarak Husni. Alichukuliwa tarehe 25/3/2018. Niliweza kuleta Taarifa hapa katika Bunge la Senati na hadi leo, habari za kijana huyu, pahali alipo, ama kama yuko hai au ashafariki hazijulikani. Haki Afrika ambayo ni kundi la haki za kibinaadamu ambayo inafanya kazi Mombasa kimeweza kutoa ripoti yake. Mpaka sasa, mwaka huu wa 2021 peke yake, kufikia tarehe 30/10/2021, watu 42 wameweza kuchukuliwa bila ya sababu yeyote. Kati ya hawa, 17 peke yake ndio wameeza kurudi nyumbani kujiunga na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kawaida. Bwana Spika, swala hili la watu kupotezwa na kuuliwa kiholela liko hai katika nchi yetu. Ni inchi ambayo tulisema inaheshimu sheria. Tuna Katiba abmbayo ni nzuri sana katika Afrika Mashariki nzima. Lakini Katiba hii, haitekelezwi kulingana na vile sheria inavyosema. Haki ya kuishi, ni muhimu sana. Katiba yetu katika Kipengele 26 inasema kwamba, kila mtu ana haki ya kuishi katika jamuhuri yetu ya Kenya”. Vilevile, Kipengele cha sita cha Civil and Political Rights ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba haki ya kuishi ni haki muhimu sana katika ulimwengu. Kwa hivyo, inchi zote zinaheshimu haki ya kuishi. Bw. Spika, hatuwezi kuwa na nchi ambayo inafungia macho maswala kama haya ya watu kupotezwa na u kuuliwa kiholela."
}