GET /api/v0.1/hansard/entries/1122001/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1122001,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1122001/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, wakati wa nyuma, haki zilipokuwa zimedhulumiwa wakati wa Serikali ya awamu ya pili ya hayati Daniel Arap Moi, mambo haya yalipo angaliwa wakati wa Serikali ya Mheshimiwa Kibaki, watu wengi ambao walifanya mambo kama haya walipelekwa Mahakamani. Rais msataafu hayati Moi pia alipelekwa mahakamani kuhusiana na haki kama hizi. Kwa hivyo, ninawaonya wale ambao hivi sasa wanaendelea kudhulumu na kuhujumu haki za binadamu. Sheria itashikana na wao wakati mmoja. Hakuna swala ambalo linaweza kupita bila kuwa na sheria itakayofuatilia kuhakikisha kwamba wale ambao wameweza kupotezwa, na kuuliwa kiholela wamelipwa ridhaa ili familia ziamini kwamba haki imeweza kutendeka. Bw. Spika, tumeona Serikali ililipa pesa nyingi kwa wale ambao walifungwa, na kuwekwa kizuizini bila kushtakiwa na wengine wengi ambao waliteswa mikononi mwa polisi. Na hii inayo endelea sasa ni ile ile iliyo kuwa inaendelea wakati wa Serikali ya mustaafu hayati Daniel Arap Moi. Kwa hivyo, wale ambao wanahusika hata kama ni Director wa Anti-Terrorism"
}