GET /api/v0.1/hansard/entries/1122003/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1122003,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1122003/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "(ATPU), Director wa I ntelligence, hakuna kitu kitakulinda wewe wakati utakapostaafu ama utakapotoka katika kazi hiyo. Sheria itapambana na wewe na siku moja itakushika na kukupeleka jela kama vile ambavyo unawatesa na kudhulumu haki za Wakenya ambao washikwa bila sheria yoyote. Bw. Spika, kwa kumaliia ninasema kwamba mapendekezo yote ambayo yametolewa, ni kweli yanaweza kufanya kazi. Lakini, pia tungependa kuwe na mwongozo kuwa wale wote ambao familia au wapendwa wao wamechukuliwa kiholela, wapate fursa ya kuelezea maswala kama haya. Hii ni kwa sababu, hivi sasa, wengi wanaogopa. Mtu anaambiwa mtoto wake amechukuliwa kwa sababu ni Alshaabab . Kwa hivyo, hawezi kuzungumza na jirani yake. Wanafaa kupewe fursa ya kuzungumza maswala haya kupitia kwa Kamati za uuiyano katika maeneo yao ama kwa vikundi vya haki za binadamu ambazo zinafanya kazi kama vile Haki Afrika, Muhuri, Uraia, KenyaNational Human Rights Commission (KNHRC) na mashirika mengi ambayo yanaweza kutoa msaada kama huu wakati wa majanga kama haya. Bw. Spika, kuna shirika la Independent Medical Legal Unit (IMLU) ambalo linafanya kazi kubwa sana kuhusiana na swala hili la watu kupotezwa kiholela. Kwa hivyo, kupatikane nafasi au kutolewe fursa ya mashirika haya yaweze kuwa na nafasi ya kuwanasihi wale ambao wameadhirika ili waziweze kuona kwamba dunia imewaacha mkono na kukata tamaa. Kwa hayo mengi, ninashukuru kwa kunipa fursa hii."
}