GET /api/v0.1/hansard/entries/1122337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1122337,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1122337/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika. Nakubaliana na alivyozungumza Mhe. Duale, kwamba tusiwe watu wanaozugumza lugha nyingine hapa na kule nje tunazungumza lugha tofauti. Siyo kuwa Wakenya hawatuoni. Kila mmoja hapa ikifika siku ya Ijumaa, anarejea mashinani na hadhara ya watu wanaomzingira si chache. Kisha hapa tuweka sheria yani sisi wenyewe kifalme falme hatufai kukaa baina ya watu wawili. Lakini tukifika kule nje, hakuna hata siku moja umesikia mtu akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kisiasa kwamba watu wapeane nafasi ndiyo wavute pumzi. Wengi hapa wamezungumza kuwa kuna matatizo katika nchi zingine ambazo idadi ya watu waliochanjwa ni kubwa. Lakini pia tukumbuke kuwa Mwenyezi Mungu alivyoamua yeye hapa vifo vyetu si vingi kama vya kule. Huku miili yetu imebarikiwa. Mhe. Spika kama unakumbuka, kuna ile Hoja yangu kwamba ni lazima nchi ifunguliwe sasa hivi. Suluhisho ni kuwa anayetaka kuingia katika Jumba hili lazima aonyeshe cheti chake kuwa amedungwa sindano ya chanjo na watu waendelee kuishi maisha yao. Kila wakati tunaketi namna hii na Wakenya wote wanatuangalia sura zetu. Ni kitu gani ama ulaghai gani tunafanya? Ni unafiki gani ikiwa tunasema hapa eti ni lazima kupeana nafasi ndani ya Bunge ilhali huko nje tunajazana na watu wengi sana?"
}