GET /api/v0.1/hansard/entries/112245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 112245,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/112245/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mungatana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": "Madam Naibu Spika wa Muda, pili, ningependa kuwashukuru wenzangu ambao tulikaa na kuzungumza chini ya Parliamentary Caucus for Reforms. Ningependa kusema kwamba walionyesha ushujaa. Nasema walionyesha ushujaa kwa nini? Kwa sababu katika vyombo vyetu vya habari, kumekuwa na mazungumzo ambayo yamekwenda kinyume na maridhiano ambayo Wabunge walikuwa wanataka. Kumekuwa na mazungumzo ambayo yameenda kinyume kabisa na ule moyo wa kutaka kuelewana. Ningependa kusema ya kwamba wote ambao tulikutana, tumesema ya kwamba jambo ni moja tu; sisi Wabunge tunafanya kazi yetu kama walivyofanya Committee of Experts (CoE). CoE walifanya kazi yao wakamaliza. Parliamentary Select Committee (PSC) ilifanya kazi yao ikamaliza. Sisi Wabunge pia tunataka kufanya kazi yetu tumalize. Njia ni mbili. Tutafanya kazi yetu kwa vita tuwe tunazungumza hapa tukiwa na hasira ama tutakaa kwanza tuelewane kisha ndio tuzungumze tukiwa na hali ya kutulia. Sisi Wabunge tumeamua kwamba, hata kama vyombo vya habari vitatutukana, ni sawa."
}