GET /api/v0.1/hansard/entries/112251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 112251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/112251/?format=api",
"text_counter": 308,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Na tena tukubaliane, tusiende mbali. Angalia nchi hapa ambazo hazina bunge wala rais. Hizo nchi zimekuwa namna gani? Sisi Wakenya tumepata bahati kubwa ya kuwa na Bunge ambalo liko na nguvu. Tujenge vitu vyetu; tuheshimu na tupatie heshima Bunge letu. Tufanye kazi yetu na tukimaliza, wananchi watafanya kazi yao. Watapiga kura kwa ajili ya kuamua maoni ya ândioâ ama âlaâ. Wananchi wakifanya kazi yao, itakuwa ni wakati wa Attorney-General kupeleka hii Katiba kwa Rais na Rais afanye kazi yake. Atie sahihi, tupate Katiba mpya. Kwa hivyo, tunawaomba ndugu zetu ambao mnaandika huko nje, tafadhali--- Tunanyekekea tafadhali, tupeni nafasi na sisi tufanye kazi yetu. Tukimaliza kazi yetu, wananchi nao wafanye kazi yao kwa Referendum. Sisi hatutatishwa na hatutaogopa! Kama Bunge, tutafanya kazi yetu!"
}