GET /api/v0.1/hansard/entries/1123218/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1123218,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1123218/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Nataka kuelezea kwamba moja ya majina haya ni la Mpwani. Hili jina linalotajwa hapa, Alfred Mutweta Mshimba, ni Mpwani. Ameweza kuregesha sehemu nyingine ya Mpwani. Hivi leo, ningependa kuwaambia hao wenye kulalamika wazungumze kwa pumzi hiyo hiyo kuhusu majina hayo. Baada ya hii, kuna Privatization Commission na sioni jina la Mpwani hata mmoja. Ningependa kuwaambia wazungumze ili watu wenu watolewe ili wawekwe watu wetu. Tena baada ya hapo, kuna Competition Authority of Kenya na, vile vile, sioni jina la Mpwani lakini naona majina mawili mawili ya makabila mengine. Ningependa kuwaambia wazungumze vile vile na kwa hisia hizo hizo ya kuwa mnataka watu wenu watolewe na kuwekwe Mpwani, Mjaluo au kabila nyingine yeyote. Hii Kenya ni ya kila mtu. Kenya sio ya mtu mmoja ama wengine. Tulikuwa tukiongea na kukohoa hapa. Tulikuwa tunazungumza hapa, sio tu katika majukwaa. Tulikuwa tunaongea hapa tukiwaambia kila siku ya kuwa mnafanya makosa dhidi ya Wakenya. Mhe. Naibu Spika, mimi nalikubali hili jina na tena nitakubali na Mkenya mwingine apewe nafasi. Hii Kenya ni ya kila mtu na kila mtu ana nafasi."
}