GET /api/v0.1/hansard/entries/1123315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1123315,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1123315/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana, Mhe.Naibu Spika wa Muda. Nami naunga mkono uteuzi wa Wakenya wanne, ikiwemo akina mama wawili na akina baba wawili. Namshukuru Mhe. Rais na kusema huu ndio mtindo wa kwamba tuwe na asilimia 50 kwa 50 ya akina mama kwa akina baba katika uteuzi. Mamlaka haya ni muhimu sana kwa sababu yatalinda wale wanunuzi ama kwa Kiingereza consumers. Pia itaangalia njia ya usawa katika mambo ya biashara na soko. Kwa sababu, wakati mwengine tunaona kuweko kwa mvutano katika mambo ya biashara ama soko. Haswa hapa Kenya tumeona ushindani wa Airtel na Safaricom. Kwa hivyo, mamlaka haya ni muhimu sana na yataweza kusawazisha na kuleta ushindani mzuri wa kuendeleza biashara na masoko kwa njia ya usawa. Mwenzangu mmoja amezungumzia swala la ndugu zetu walemavu. Nami pia nataka kutia mkazo ya kwamba, wakati tunafanya uteuzi Mhe. Rais awafikirie sana hawa ndugu zetu walemavu. Jambo lingine nataka kusema ni kwamba, ni wakati mwafaka Mhe. Rais apige darubini na kuangalie jamii ambazo zimekuwa chache katika uteuzi wa sekta zetu za umma ama za kiserikali ndiyo zipewe kipau mbele. Akifanya hivyo, tutaweza kuwa na usawa tunaozungumzia katika Katiba yetu wa akina mama, kijamii na wa sehemu zote za taifa la Kenya. Nasema hivyo kwa sababu najua mpaka sasa kuna jamii ambazo uwakilishi wao katika sekta za kiserikali, nafasi za kuweka maamuzi katika serikali na uwakilishaji wao bado ni mchache. Hivyo basi, tuweze kuwapatia kipau mbele jamii kama Waturkana, Wadorobo, Wamijikenda, Wabajuni, na zile zinazotoka kule kaskazini na kusini; Wamaasai na Wasamburu. Tuweze kuangalia jamii hizi ambazo bado ni chache katika sehemu za kufanya maamuzi ama katika sekta za umma na zipewe kipau mbele. Hili litawezekana iwapo tutakuwa na takrimu mahususi za ukweli za kuonyesha tunafanya ama kutekeleza vipi Katiba yetu ambayo tuliipigia upato. Ili kuhakikisha ya kwamba kutakuwa na uwakilishaji ambao utachukua sura ya Kenya na kusawazisha historia za nyuma ambako kulikuwa na jamii zilizotengwa ama ni chache. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}