GET /api/v0.1/hansard/entries/1123316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1123316,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1123316/?format=api",
"text_counter": 360,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Nataka kumshukuru Mhe. Rais pia kwa ile Tume ya Ubinafsishaji lakini niwaambie wale Makamishna tafadhali Bandari ya Mombasa isifanyiwe Ubinafsishaji. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu na kuseme kuwa wakati huu akina mama nafikiri tumepata mavuno katika uteuzi. Mhe. Rais, mtindo ubaki huo huo na akina mama tuwe mbele katika nyanja za uongozi sawia na akina baba na sambamba katika maamuzi na ujenzi wa taifa la Kenya. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu walioteuliwa wote katika tajiriba ya kielimu na ya uzoefu wa kazi wamefuzu. Pia, katika Sura ya Sita ya Katiba, hawana jinai wala makosa ya uhalifu. Hatukuona memorandamu yoyote ambayo imewapatia kashifa ama imesema hawa walioteuliwa wana makosa fulani. Kwa hivyo, mimi naunga mkono, mia asilimia. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}