GET /api/v0.1/hansard/entries/1123392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1123392,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1123392/?format=api",
"text_counter": 436,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Naunga mkono Ripoti hii ya Kamati kwa sababu lazima kuwe na kanuni haswa za kuangalia kama maziwa mbadala yatasaidia mtoto na yako na madini yanayohusika na yanayohitajika. Pia sasa hivi tunaona katika soko kumetokea maziwa sampuli tofauti tofauti ambazo wakati tunapatia watoto zinaleta shida haswa shida za maradhi ya tumbo. Kwa hivyo, lazima tuwe na njia ya kuangalia kama hayo maziwa mbadala ambayo yameingia katika soko zetu ni yale ambayo yamemulikwa na kuangaliwa na madaktari - haswa wale wanaosimamia afya ya watoto - ili tuwakinge watoto wetu dhidi ya maradhi yanayotokana na maziwa hayo. Vile vile, lazima tuangalie bei kwa sababu wakati mwingine unapata mzazi amezaa mapacha watatu ama watoto watano kwa mpigo mmoja. Tumeona mzazi amezaa mapacha saba kwa wakati mmoja ila hizo bei haziangaliwi. Hakuna kanuni za kuangalia bei hizo kuhakikisha kuwa ni rahisi kwa mzazi ambaye ana mtoto mchanga kupata maziwa mbadala ya kumfidia mtoto wake. Ni kama jambo hili ni ndogo sana lakini ni jambo la msingi. Hii ni kwa sababu ikiwa mtoto hatapata madini fulani akiwa mchanga kupitia maziwa yanayotoka kwa mama, lazima tujue kuwa maziwa mbadala yatakuwa na yale madini yanayohitajika. Maziwa ya mama huwa siku zote yanakinga dhidi ya maradhi na humwezesha mtoto kukua kwa kasi na kwa hali bora zaidi. Hivyo basi, hilo ni swala nyeti ambalo lazima Wizara ya Afya iweke mikakati na kanuni za kuhakikisha kwamba ni muhimu sana. Vile vile, lazima kina mama wazazi wafunzwe ili waelewe kuwa wakati mzazi amekosa maziwa ama imekuwa shida kwa sababu fulani kupata maziwa ya kutosha, wajue ni sampuli gani za maziwa mbadala ambazo zitasawazisha yale maziwa haswa ya kutoka katika titi la mama. Kwa hivyo, ni lazima mambo kama hayo yafanyike. Ni muhimu kuwa zile programmes ambazo zilikuwa zikifanyika zamani za kupitia mashinani na kuzungumzia akina mama katika zahanati za mitaani ama za mashinani ziendelee. Lazima suala kama hili lipewe kipaumbele ili akina mama wazazi wawe sawa na pia wawe na elimu ya kuwanyonyesha watoto. Mzazi anahitajika kumnyonyesha mtoto kwa takriban miaka miwili na siyo chini ya hiyo. Lakini iwapo kuna matatizo, basi inafaa watoto wapate maziwa mbadala kwa takriban miaka miwili ama zaidi, lakini si chini ya hiyo. Hii ni kwa sababu mtoto akiwa chini ya umri wa miezi sita, hawezi kula chakula kingine isipokuwa maziwa. Kwa hivyo, lazima tutilie akilini maziwa mbadala na kuweka kanuni kwa sababu iwapo mtoto wa umri wa miezi sita na chini amekosa maziwa ya mama, hataweza kula chakula kingine. Lazima tupate maziwa mbadala ambayo yana madini yanayohitajika. Lazima tuwe na kanuni za kuangalia masoko yetu kuhusu bei na kuona ni maziwa gani haswa yatakayokubalika kulingana na sheria za kiafya kupitia Wizara ya Afya pamoja na zile taasisi ambazo zinahusika na mambo ya watoto ama ukuzaji wa watoto. Kwa hayo, naunga mkono sana Ripoti ya Kamati inayozungumzia suala hili. Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}