GET /api/v0.1/hansard/entries/1124420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1124420,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1124420/?format=api",
    "text_counter": 508,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunakumbuka vizuri kuwa si zamani ambapo Rais wetu mpendwa, Mhe. Uhuru Kenyatta, alichukua ahadi kwamba atapiga vita ukatili dhidi ya jinsia. Kwa sababu hiyo, tunafaa kuipa tume hii nguvu ili iweze kupigana vita hivyo. Tunafaa kutafuta mbinu ambazo zitaipatia tume hii nguvu ili ipigane vita hivi vita. Kwa mfano, kila kituo cha polisi chafaa kiwe na dawati la kijinsia. Ukitembea, utapata kuwa bado sehemu zingine hazina polisi mwanamke au hilo deski halina nguvu. Ukifika na kuuliza kwa nini mambo yako hivyo, utaona hawako au hakuna mtu wa kuwa hapo. Mbinu nyingine za kuongeza nguvu kwa hizi tume ndio zisiwe tu tume pale, ni kuhakikisha kuwa ziko na pesa na uwezo wa kufanya kazi yao. Pia, tume inafaa kuhakikisha kuwa ikiajiri maaskari, wanawake wawe wengi. Tume inaweza kuwa pale, lakini haina uwezo wa kufanya haya mambo. Kwa mfano, ukichagua wanawake wengi wapelekwe kama kule kaunti ya Lamu ambapo maaskari wanawake ni kama 10 peke yake, ilhali wengine wote ni wanaume. Wale watu wa kupambana na madawa ya kulevya huambiwa na wanawake wasiwakague na kumbe wameficha madawa ya kulevya mwilini. Kwa hivyo, tume inafaa kupewa nguvu ndio wapatie wale maafisa nguvu ya kupigana na vita hivi vya dhuluma za kijinsia."
}