GET /api/v0.1/hansard/entries/1125997/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1125997,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1125997/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa hii nafasi nichangie huu Mswada. Ninaunga mkono huu Mswada kwa sababu unaongea juu ya vikundi vya akina mama na sisi wote tuko kwenye Bunge hili tuwakilishe wanawake. Wanawake tunao wakilisha wamejiunga na vikundi mbalimbali. Kuna muungano wa wanawake unaohitaji wawe kwenye vikundi vya watu mia moja vinavyojiita community based organisations . Pia, kuna vikundi ambavyo vinahitaji watu 20 ili visajili wanawake. Ninaunga mkono huu Mswada kwa sababu hatuna sheria zinazohusu utekelezaji wa mambo yanayohusu kina mama. Huu Mswada ukiwa sheria, kina mama watajua vikundi vyao ama muungano mkubwa ni nini. Wakishaelimishwa, watatofautisha mahali pa kupata pesa, vile watazipata hizo pesa na maelezo kuhusu vikundi ambavyo wamejiunga na kusajili. Wanawake wengi katika nchi yetu hawajaelimika kuhusu vikundi vya akina mama. Wengi wamekuwa na shida ya jinsi ya kujiunga na hivo vikundi. Tunazungumzia akina mama walioenda shuleni ambao wana elimu na pia wale ambao hawajaenda shuleni. Wote ni wamama na wanahitajika kuunda vikundi vyao ili wafaidike na pesa za Serikali. Ninaelewa kwamba kuna vikundi fulani katika nchi yetu vinavyopatiana pesa kwa vikundi vya wamama na vijana, lakini hakuna sheria ya utekelezi wa mambo yao. Kina mama wengi wameumia baada ya kuchukua pesa kutoka kwa vikundi visivyo na sheria tekelezi nchini Kenya. Kuna pesa za shylock zenye akina mama hawaelewi. Kina mama wanaumia sana wanapochukua hizo pesa kwa sababu hawana elimu ya kutosha. Tunapounga mkono Mswada huu leo, ninataka kuhakikishiwa kuwa kutakuwa na waalimu katika kila eneo la Bunge ili kina mama wapate elimu ya kutosha. Kuna pesa za Uwezo Fund zilizo chini ya kila Mbunge ilhali kina mama wengi hawajui. Pia, tuko na Women Enterprise Fund ambayo yote ni pesa za Serikali lakini kina mama wengi hawana elimu wala habari kuhusu watakavyo tafuta hizo pesa na utaratibu wake. Kwa hivyo, tukiwa na sheria kama hii, kina mama watafaidika sana. Nimeskia Mjumbe mmoja akisema kuwa wanaume wamekuwa wakilalamika mbona vikundi vya kina mama vinapewa kipao mbele kwa kila jambo lakini hawajui kuwa wazee hawajakatazwa kujiunga na vikundi vya kina mama, lazima kuwe na asilimia thelathini ya wanaume. Wote wanataka kuelimishwa. Ninatarajia tutakapotengeneza hii sheria, Serikari yetu itakuwa na uwezo wa kuhakikisha kwamba kutakuwa na mwalimu katika kila eneo la Bunge ili kina mama wapate elimu ya kutosha. Pia, tuko na vikundi vya vijana na wasiojiweza. Hawajui kuna habari nzuri ya kuwa kuna pesa za Serikali. Ninapongeza nchi ya Kenya maana ni moja katika Bara la Africa ambayo imetenga pesa kwa vijana, kina mama na watu wasiojiweza. Kuna pesa zisizo na riba za NationalAffirmative Action Fund (NGAAF ) ambao sisi Waakilishi wa Kaunti tunasimamia. Kina mama wengi hawafahamu kuwa hizi pesa zinazosimamiwa na Mwakilishi wa Kaunti zina utaratibu na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}