GET /api/v0.1/hansard/entries/1125998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1125998,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1125998/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": "sheria zake. Hawawezi kutafoutisha na wale shylocks ambao wamekuwa wakinyemelea kina mama pale nyumbani kwa sababu hawana mafunzo ya kutosha na wamekuwa wakiumia sana. Ninaamini huu Mswada utatunga sheria tosha na jambo la maana ni elimu kwa kina mama. Kina mama na wazee watapata elimu. Haijasemwa kuwa kikundi kikiwa ni cha kina mama wazee hawatakikani kujisajili. Kinachohitajika ni mafunzo. Ikisemekana ni kikundi cha kina mama, wanaoongoza ni kina mama lakini theluthi chache ya wazee wanafaa kujisajili. Itakuwa ni vizuri tukiwa na sheria ya kina mama katika nchi yetu maana ni watu wenye bidii. Kina mama wakipewa pesa ama wakisaidiwa kwenye mambo ya elimu kuhusu jinsi ya kutengeneza vikundi vyao pale nyumbani watafaidika sana. Tutafaulu maana mambo yote tutakuwa tumeanzia pale chini. Ukisikia mara nyingi tukisema mambo ya “ bottom up ” ama kuelimisha watu na kuwapea usaidizi kutoka chini, imekuwa ikiendelea lakini lazima sasa isizitishwe na sheria. Kwa hivyo, mimi kama Mwakilishi wa Kaunti ya Nakuru nina hakika ninasikilizwa na wale walionichagua. Sheria ambayo imetoka sasa itasaidia kina mama. Kuna kina mama ambao wamefiwa na wazee ama pia wazee wamefiwa na bibi zao. Nina hakika huu Mswada utawagusa na kuwaelimisha vile tunawezajenga uchumi wetu kutoka pale vijijini kuja juu. Ninaunga mkono huu Mswada. Pia, ninampongeza Mbunge wa Suba Kaskazini kwa kupambana na Mswada huu wa leo wa Gender Commission . Ningependa kumwambia Mheshimiwa kuwa nimekuwa nikipenda mjadala wake lakini Gender Commission imekuwa mjini Nairobi tu. Kwa hivyo, lazima kufanye devolution na kina mama pale chini wajue kazi ya hii"
}