GET /api/v0.1/hansard/entries/1126004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1126004,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1126004/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ni kweli na imekuwa pigo kubwa mno. Leo itakuwa ni siku ya nne tangu tuwapoteze wapenzi wetu Ali Omar Naaman, Carol Wayua, Elysian Musyoki na Athman Mohammed. Leo tunazungumzia sharia, jinsi vikundi vinafaa kusajiliwa na vile vitaifadhika. Kati ya wale wangehusika zaidi ni hao tayari, wameenda mbele za haki. Kwa Allah tunatoka na kwa hakika, kwake tutaregea. Ninaomba Mwenyezi Mungu atujalie sote tuwe na subra katika wakati huu wa huzuni. Kila nafsi itaweza kuonja kifo. Leo wametangulia nasi tuko nyuma yao. Leo, tunazungumzia kuhusiana na sheria ya jinsi vikundi vitasajiliwa. Kuna kitu hapa kimenifurahisha Zaidi. Kuna baadhi ya vikundi vingine vinaweza kujisajili wakiwa Mombasa kisha mwingine aenda kujisajili pia katika sehemu nyingine. Utapata vile vikundi vina jina moja. Kuna uwezekano wa kuhadaa, na fedha zizizofaa kwa mtu fulani zikachukuliwa kwingine. Pia vile vile, utapata kuwa tukiwa na sheria ya jinsi ya vikundi hivi, watu wataweza kustirika kwa ubaya wa nje na kwa wao wenyewe kwa wenyewe. Sisi kule kwetu tunasema kwamba pesa haikuslimu, yani hii shilingi inaweza kufanya jambo lolote."
}