GET /api/v0.1/hansard/entries/1126051/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1126051,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1126051/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Asha Hussein",
"speaker": {
"id": 13262,
"legal_name": "Asha Hussein Mohamed",
"slug": "asha-hussein-mohamed"
},
"content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu wa kusajili makundi ya jamii. Tuna makundi tofauti tofauti katika jamii zetu, haswa katika Kaunti ya Mombasa. Tuna makundi yaliosajiliwa lakini hayana uwezo wa kuendeleza shughuli zao na yanapopata pesa za Serikali huwa yanazifuja vibaya. Kwa hivyo, naunga mkono usajili huu kwa sababu makundi hayo yatakuwa yanafuatiliwa ili yaweze kujiendeleza yenyewe kiuchumi, yaendeleze miradi yao mbali mbali na kujimudu kimaisha. Kwa hivyo, naunga mkono haya makundi kwa sababu tunapoelekea, tunataka makundi hayo yapewe pesa nyingi zaidi kwa sababu ya ubunifu wa kufanya miradi. Yanaweza kuvumbua miradi mipya tofauti ili yapate pesa nyingi kutoka kwa Serikali. Naunga mkono usajili wa makundi hayo ya kijamii. Asante sana, Naibu Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}