GET /api/v0.1/hansard/entries/1126099/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1126099,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1126099/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": " Shukrani Bi Naibu wa Spika wa Muda kwa kinupatia fursa hii ili nichangie Hoja hii ambayo ni muhimu sana. Unajua ya kwamba swala la mashamba ni swala nyeti, hasua hili ambalo tunaliongelea sasa ni swala ambalo limesumbua jamii sana kwa muda mrefu. Nachukua fursa hii nipongeze kamati husika kwa kazi ambayo wameifanya. Nimeona walitembea kule wakawasikiza wananchi, wakapata fursa pia ya kumsikiza mwenye shamba yule na wakasikiza pia wahusika mbali mbali ikiwemo serikali ya Kaunti yetu. Nikiangalia hii ripoti, ninashukuru kwa mambo kadha wa kadha. Kwanza, ni kwa sababu ya ile shamba ambayo imepeanwa kwa ajili ya wananchi ambao walikuwa wanagadhabika na hawapati usingizi kila siku wakifikiria kwamba wanaweza kuja kufurushwa mahali au sehemu ambazo wameishi kwa muda mrefu. Pia nashukuru kwa ajili ya kile kipande cha shamba ambacho kimetolewa kwa ajili ya shule. Kwa kweli ilikuwa ni ghadhabu kwamba shule inasemekana ni ya mtu binafsi na ikaleta utata sana na pia kwa kuruhusiwa kutumia zile barabara ambazo zilikuwa zinaleta utata. Zinafungwa na wananchi hawawezi kuzitumia kwa sababu ziko kwa sehemu ya mtu binafsi. Nashukuru kwamba zitaenda kuachiliwa zirudi kwa wananchi. Kwa hilo napongeza Kamati sana. Kwa sababu ya hali halisi iliyoko kule pia, ningependa kuunga mkono sana kwamba hizi lease wakati zinapoisha ni muhimu kuhusisha jamii na ni muhimu ziweze kurudi kwa wananchi kwa sababu watu wameteseka sana kwa mabwanyenye fulani ambao wameingilia watu wadogo ambao mara nyingi wanawaita maskwota. Watu wamedhulumiwa sana. Mashamba ambayo yalikuwa ni ya mababu zao yamekuja kupotea kwa sababu hizi lease zinakuwa renewed mara kwa mara na basi watu wamekosa fursa ya kupata sehemu za kuishi, kufanya ufugaji au hata za kulima."
}