GET /api/v0.1/hansard/entries/1127684/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1127684,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1127684/?format=api",
    "text_counter": 578,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuzungumzia mambo ya wale watu ambao wamestaafu katika nafasi mbalimbali nchini. Ningependa kumshukuru Mhe. Didmus Barasa kwa kuleta Mswada huu katika Bunge hili ili wale watu ambao wamestaafu, mahali popote walipo, wapate nafuu. Kuna watu wengi waliokuwa wakifanya kazi na wakastaafu, haswa walimu na wale waliokuwa wakifanya kazi katika Idara ya Posta na Reli. Hadi sasa, watu hao hawajalipwa pesa zao za kustaafu. Iwapo tutakuwa na marekebisho haya ya kuhakikisha kwamba wale wanaostaafu wanapata haki yao, itakuwa ni vyema kwa sababu wengi wanaumia sana na wengine wana watoto ambao hawaendi shuleni kwa sababu ya kukosa karo. Katika sehemu za Trans Nzoia, kuna watu ambao wamestaafu na wanaumia. Wengi wao wanashindwa kupambana na changamoto na wanaamua kwenda kwenye vinywaji wakipoteza maisha yao. Ningependa kuzungumzia Shirika la Telkom kwa sababu nilikuwa mfanyikazi kule. Wengi waliostaafu wamepoteza maisha yao kwa sababu ya maisha duni. Wengi wameamua kwenda kukaa penye kuna vinywaji na mwishowe wamepoteza maisha yao na watoto wao hawaendi shule. Inakuwa ni aibu sana kuona mtu aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ama mtu aliyefanya kazi katika Idara ya Telkom akiumia mno. Iwapo Mswada huu utapitishwa, utasaidia watu wengi kupata nafuu. Ningependa pia kuzungumzia serikali za kaunti. Hapo awali, nilikuwa Mwakilishi Wadi. Wafanyakazi katika municipality na wale wa county councils wanaumia kwa sababu hawajapewa pesa zao za kustaafu. Huu Mswada utasaidia watu wengi sana ambao wanaumia. Vile vile, ninafikiria kuwa itakuwa ni jambo nzuri mno iwapo tutaweza kubuni maeneo ya kupeleka hizi fedha kwa watu wanaotoka sehemu hizo. Nakushukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda na pia ningependa kumshukuru Mhe. Didmus Barasa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}