GET /api/v0.1/hansard/entries/1127687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1127687,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1127687/?format=api",
"text_counter": 581,
"type": "speech",
"speaker_name": "Masinga, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Joshua Mwalyo",
"speaker": {
"id": 13423,
"legal_name": "Joshua Mbithi Mwalyo",
"slug": "joshua-mbithi-mwalyo-2"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hata nami nitaongea kwa Kiswahili leo. Hata mimi ningependa niongeze ya kwamba huu ni Mswada wa maana kabisa. Mtu akifanya kazi kwa muda mrefu, anatakikana apate kile chake na kweli afurahie siku zake za uzeeni. Utakuta kwamba ikiwa mtu alikuwa amezoea mshahara kila mwisho wa mwezi na sasa haupati, maisha yake hudhoofika na pia huwa na changamoto nyingi kwa sababu amefikisha miaka 60. Hiyo ndiyo ile miaka ambayo Biblia inasema ni ya magonjwa na udhaifu. Kwa hivyo, itakuwa ni kitu cha maana ikiwa mtu atapata pesa zake za uzeeni. Tukipitisha huu Mswada, utakuwa ni wa kusaidia sana sana wale watu ambao wanafanya kwa mashirika mbalimbali ambayo hukataa na pesa zao. Sana sana, watu ambao walifanya kwa county councils zile za zamani bado wanadai pesa zao. Hawazipati na zinapotelea hapa na pale. Niko na watu wengi kwa constituency yangu ambao mpaka sasa wanafuata hiyo pesa. Kwa hivyo, ingekuwa jambo la msaada kama tunaweza kupitisha Mswada huu."
}