GET /api/v0.1/hansard/entries/1127697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1127697,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1127697/?format=api",
"text_counter": 591,
"type": "speech",
"speaker_name": "North Imenti, JP",
"speaker_title": "Hon. Rahim Dawood",
"speaker": {
"id": 2572,
"legal_name": "Abdul Rahim Dawood",
"slug": "abdul-rahim-dawood"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningetaka kuunga Mswada huu wa Mheshimiwa Didmus Barasa mkono. Kuna shida katika Kenya yetu kuhusu pesa za uzeeni. Wakati mtu anakatwa pesa zake ni harusi. Lakini wakati wa kulipwa ni matanga. Wakati tunapeana pesa za uzeeni ama pension, huwa tunakatwa kila wakati na kila mwezi. Wakati tunaenda kudai pesa hizo, unaweza kupata mtu ameenda kwa maofisi leo na kesho na hata miaka. Kuna wakati nilikuwa nimeleta Swali kwamba kulikuwa na mzee alikuwa anataka pesa zake. Alikuwa amekaa miaka kumi akija Nairobi kutafuta hizo pesa na hakuzipata. Kuna insuarance zimefanywa na Wizara ya Interior and Coordination ofNational Government za polisi. Watu wamepoteza hata maisha. Utapata mtu amekuwa kwa Idara ya polisi na amekufa bila hizo pesa. Hata sasa, familia yake haijalipwa fidia. Hawapati pesa kabisa. Ni shida kwa sababu inasemekana wako kwa Pioneer Insurance huku wamefanya kazi katika Kenya Reinsurance Corporation Limited (Kenya Re). Ukiuliza kwa Idara ya Fidia ya Polisi, wanasema kwamba wanangojea pesa itoke KenyaRe. Lazima tuone hili ni jukumu la kila kitengo cha Serikali kujua ni nani atalipwa fidia ama pesa za uzeeni. Naunga huu Mswada mkono. Upitishwe kwa haraka ndio watu wapate pesa kwa haraka."
}