GET /api/v0.1/hansard/entries/1127699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1127699,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1127699/?format=api",
"text_counter": 593,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nami naungana na wenzangu kuchangia marekebisho haya huku nikimpongeza Mhe. Barasa kwa kuleta haya Bungeni. Nataka kwanza tujiulize ikiwa haya tunayojadili hapa Bungeni leo ni ya sheria ambayo tayari iko katika nchi hii ama haiko. Ukweli ni kwamba hii ni sheria tayari ipo lakini imemlazimu Mhe. Barasa kuiregesha Bungeni kwa sababu ya marekebisho. Nataka tujiulize kwa nini imelazimu irudi Bungeni kwa sababu ya marekebisho. Hali halisi ni kwamba sheria hii inawagandamiza na kuwadhulumu Wakenya sana. Wengi wameenda mbele za haki bila kupata hizi haki zao. Unapokuwa mfanyikazi na kila mwisho wa mwezi unakatiwa pesa unazowekewa ukiambiwa ni pesa ya uzeeni, la kushangaza ni kuwa unapozihitaji zile pesa hupati. Inawagharimu Wakenya wengi kwa sababu wakati zikifika, huwa tayari wamezitumia kwa gharama za kusafiri kutoka mashinani kuzifuata pesa mahali zilipo. Ukweli ni kwamba haya ni matatizo na hizi ni dhulma na sio sawa. Hali hii imewafanya Wakenya kuwa wadhaifu na wanyonge sana. Mtu anapoona picha hii kwa mwenzake wakati yeye ako kazini, anajihisi na yeye atakuwa kama yule. Leo niko kazini na ninachokipata ni gharama zangu na familia yangu. Hakuna kile ambacho naweka kama akiba. Lakini kwa thamana kubwa, watu wakubali kuwekewa hizi pesa kwa sababu wanajua zitawasaidia katika maisha ya uzeeni kwa kuendelesha maisha yao. Hili limekuwa changamoto; haliwasaidii Wakenya. Na haya lazima tuyazungumzie kwa ukweli. Kwa sababu hiyo, ningependa Bunge hili, katika kurekebisha Mswada huu, liseme kuwa ile siku mtu anapewa barua yake ya kustaafu, ndio siku hiyo pesa yake awekewe kwa akaunti yake kwa benki. Sio eti wanakupa barua yako ya kustaafu, unanenda nyumbani halafu unaanza kuitisha malipo yako za uzeeni baada ya miaka miwili au mitatu. Hivyo sio sawa. Serikali inajua wakati mtu anastaafu. Pesa zake zafaa kushughulikiwa mapema. Siku unapewa barua yako kwenda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}