GET /api/v0.1/hansard/entries/1127700/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1127700,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1127700/?format=api",
"text_counter": 594,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "nyumbani, wafaa kuambiwa pesa zako ziko benki uende ukachukue. Ndiyo ujue utazifanyia nini. Sioni sababu hata moja ya pesa hizi kukaa katika sehemu ambazo zipo kwa muda wote huo, kama miaka mitano au sita au saba, baada ya mtu kustaafu. Baada ya hizo siku zote, pesa hizo zinazalisha riba katika benki. Lakini mtu yule hapewi! Wanaochukua riba ni watu wenngine Serikalini. Ndiposa utapata matatizo makubwa katika idara hizi. Kuna masuala mengi. Wengi wanapatikana na makossa ya ulaghai na ufisadi katika idara hizi kwa sababu wamezuia haki za watu wakidhania labda ni haki zao. Kwa hivyo, la usawa katika kurekebisha haya matatizo ni ihakikishiwe Wakenya ya kwamba siku wanapostaafu ndio siku wanapewa haki zao. Hili ndilo litakuwa usawa wa marekebisho ambao tutafanya. Ikiwa sheria ipo lakini sheria yenyewe ni ya udhalilifu na usumbufu kwa Wakenya, haitakuwa na maana Bunge hili kufanya marekebisho kwa namna itakvyozunguzwa bila kupatikana suluhu ambayo itakuwa ni usaidizi na italeta nafuu kwa Wakenya. Kwa hayo machache, Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono merekebisho haya na kumpongeza Mhe. Didmus kwa kuyapendekeza."
}