GET /api/v0.1/hansard/entries/1127716/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1127716,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1127716/?format=api",
"text_counter": 610,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Mfanyikazi wa taifa ni mtu ana wajibu muhimu katika ujenzi wa taifa la Kenya. Mfanyikazi yule anaheshimika pindi ako hai. Anapokufa, ndiyo tunatuma salamu za rambirambi zetu. Hakuna ajuae wajane na mayatima. Haki ya yule aliyekufa si haki tena mpaka watu wa Bima watakapopenda. Sheria hii iliyorekebishwa na Mhe. Barasa itawanasua wale wanyonge waliodhulumiwa. Malipo ya uzeeni imekuwa ni kama dhuluma katika nchi ya Kenya. Kwa kawaida, miezi sita kabla ya kustaafu kwake, mfanyikazi huwa anapewa habari kwamba anakwenda kustaafu. Kwa nini shughuli za kumlipa yule mfanyikazi zisianze wakati huo? Wengine wamengojea pesa za uzeeni hadi wakafa. Ningependa kwa ushahidi kamili nikwambie kinachoendelea kwa mambo ya bima si ufisadi! Ni wizi!"
}