GET /api/v0.1/hansard/entries/1128460/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1128460,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128460/?format=api",
"text_counter": 727,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "kuuona pahali pengine. Ni mchanga mweusi na unanga’ra sana. Lakini hizi taasisi zetu hazina nguvu hizo za kufika sehemu hiyo na kuangalia kiini cha jambo hilo. Hata kijiji hicho kimeitwa Mtangawanda kwa sababu ya huo mchanga mweusi. Inaweza kuwa mchanga huo ni madini au vitu muhimu ambazo ziko hapo na labda zingeinua sehemu hiyo. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kuna watu wengine wanatuchekesha sana. Wanasema toroli au wheelbarrow ni utafiti. Ni utafiti aje? Nyanyangu ametumia wheelbarrow. Nyanyake nyanyangu, alitumia wheelbarrow. Ni kitu gani kipya kiko hapo ? Utafiti unafaa ufanywe na kama ni kutengeza toroli, ziwe ni za kimbinu za kisasa. Angalau angekuja na toroli ambayo ina mbinu ya kitofauti na zile nyanyangu au babu yangu alitumia. Lakini hizo hizo na tunaambiwa ni utafiti, tunafaa kupatia taasisi hizi mbinu ili wakenya waweze kulinganishwa na nchi zingine zinazounda vitu. Sisi wakenya tumesoma baada ya COVID-19. Hatukuwa tunatengeza barakoa lakini sasa hivi, Kenya inatengeza barakoa."
}