GET /api/v0.1/hansard/entries/1128696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1128696,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1128696/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kamukunji, JP",
"speaker_title": "Hon. Yusuf Hassan",
"speaker": {
"id": 398,
"legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
"slug": "yusuf-hassan-abdi"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kutoa Arifa ya Hoja kuwa: Tukitambua kifungo cha 7 cha Katiba ya Kenya kimebainisha lugha ya Kiswahili ni lugha pekee ya kitaifa na pia ni lugha rasmi pamoja na Kingereza katika nchi ya Kenya; aitha Serikali imepewa wajibu wa kulinda na kuendeleza lugha tofauti za watu wa Kenya na kukuza matumizi ya lugha za kiasili nchini; tukitanahabi kwamba Kiswahili ni mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Nchi za Africa, na hivi majuzi tu Umoja wa Mataifa pia umeweka siku maalum, tarehe 7 Julai, kama siku ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili kote duniani; na pia Vifungo vya 119 na 137 vya Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Serikali na Dola za Afrika Mashariki zimewajibika kustawisha na kuendeleza lugha ya Kiswahili kama lugha ya umoja katika nchi za Afrika Mashariki."
}